Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 24 Novemba, 2017

Thibaut Courtois
Golikipa wa Chelsea, Thibaut Courtois anaweza kuhamia kati ya, Juventus, Real Madrid, PSG au Atletico Madrid.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amekataa ofa ya Arsenal ya paundi milioni 40 kwa Karim Benzema, akidai ni aibu.

Eliaquim Mangala amekiri kwamba, anaweza kuondoka Manchester City ili kupata nafasi ya kutosha uwanjani. (Sun)

Glenn Murray anasema angepewa heshima kubwa zaidi kwa kiwango chake akiwa na Brighton endapo angekuwa na jina la kigeni.

Gary Megson
Meneja wa muda wa klabu ya West Brom, Gary Megson anasistiza kwamba mechi yake ya kwanza kama kocha wa klabu hiyo dhidi ya Tottenham, hatakuwa kigezo kwa yeye kupewa kazi ya kudumu. (Telegraph)

Wayne Rooney ameitaka bodi ya klabu ya Everton kumaliza tofauti zilizopo kati yao na wafanye uteuzi wa meneja mpya wa klabu hiyo kufuatia kuchapwa bao 5-1 na klabu ya Atalanta.

Klabu ya Barcelona iko tayari kushindana na klabu ya Real Madrid kuwania saini ya beki wa Athletic Bilbao, Aymeric Laporte. (Express)

Eden Hazard amekiri kwamba, anaipenda klabu ya Real Madrid, lakini hana nia ya kuiahama klabu ya Chelsea.

Mesut Ozil anataka mshahara wa paundi 330,000 kwa wiki Barcelona, ambao wanataka kumuuza Arda Turan kupata fedha kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa klabu ya Arsenal.

Marouane Fellaini
Klabu ya PSG iko mstari wa mbele katika kinyang'anyiro cha kutafuta saini ya Marouane Fellaini kama atachagua kuondoka Manchester United, na iko tayari kumpa mkataba wa miaka minne.

Klabu ya Rennes inafukuzia kumnasa mshambuliaji wa Leicester, Islam Slimani kwa mkopo, lakini inakumbana na ushindani kutoka Watford na Crystal Palace.

Burnley inamfuatilia kwa karibu zaidi nyota wa klabu ya Kilmarnock, Jordan Jones mwenye umri wa miaka 23 kuelekea dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Daily Mail)

Mohamed Salah
Kuelekea mechi ya Liverpool dhidi ya Chelsea Jumamosi, Eden Hazard amekiri kwamba, mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah hakupata nafasi ya kufanya vizuri akiwa na Chelsea. (Guardian)

Chris Coleman amempa nafasi kubwa Craig Bellamy kurithi nafasi yake kama meneja wa Wales.

Riyad Mahrez anafurahia Demarai Gray kupewa nafasi katika klabu ya Leicester, kwani anahisi kwamba, winga huyo ana msaada mkubwa kwa klabu. (Star)

Henrikh Mkhitaryan na Jose Mourinho
Henrikh Mkhitaryan aliachwa nje na Jose Mourinho ikiwa ni mipango ya kumfanya aongeze bidii kufuatia kuwa na mwanzo mbaya msimu huu.

West Ham wako tayari kuingia vitani dhidi ya klabu ya Crystal Palace kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Bournemouth, Harry Arter.

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya West Ham, Jermain Defoe ameiambia klabu yake ya zamani impe nafasi David Moyes.

Jack Wilshere amekiri kwamba, anaweza kutakiwa kuondoka Arsenal ili apate nafasi ya kotosha uwanjani.

Gabriel Jesus
Gabriel Jesus anasema anaitazama kwa makini rekodi ya mchezaji mwenzake wa Manchester City, Sergio Aguero, licha ya kwamba nyota huyo wa Argentina ameiweka rekodi hiyo mwezi uliopita.

Klabu ya Derby inataka Joe Ledley asaini mkataba mpya klabuni hapo, lakini Sunderland ina matamanio makubwa ya kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa mika 30. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 24 Novemba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 24 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/24/2017 03:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.