Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 21 Novemba, 2017

Marco Asensio
Nyota wa Real Madrid, Marco Asensio yuko tayari kujiunga na klabu ya Chelsea kama hatapewa nafasi ya kutosha Bernabeu.

Mark Noble amewaomba mashabiki wa West Ham wenye hasira kuiunga mkono timu yao wakati huu ambapo iko inapigania isishuke daraja EPL chini ya kocha mpya, David Moyes.

Nyota wa Barcelona, Ousmane Dembele anatarajiwa kurejea kutoka majeruhi kwenye mechi ya 'El Clasico' dhidi ya Real Madrid mwezi ujao. (Express)

David de Gea
Klabu ya Real Madrid iko tayari kulipia kiasi cha paundi milioni 70 kumnasa goli kipa wa Manchester United, David de Gea.

West Brom wanamtaka Sam Allardyce aje kuwaokoa baada ya wachezaji kadhaa wakionekana kutofurahishwa na kuondoka kwa Tony Pulis.

Ronaldinho anasema kwamba Pep Guardiola atafanya kile alichokifanya akiwa Barcelona katika klabu ya Manchester City.

Winga wa klabu ya Watford, Richarlison ambaye tayari yuko kwenye mikakati ya klabu ya Tottenham, amekuwa kivutio kikubwa China.

Marco Silva
Marco Silva anaweza kuwa mstari wa mbele kuchukua nafasi ya meneja Everton lakini aliyekuwa kocha wa Manchester United, Louis van Gaal anaonekana kuwa miongoni mwa wanaoitaka nafasi hiyo kwa sana. (Mirror)

Joel Matip anategemewa kuwa 'fit' kwa ajili ya mechi ngumu ya Liverpool ya Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea.

Rashford anasistiza kwamba, Jose Mourinho anaipitisha Manchester United kwenye njia sahihi kuifanya Old Trafford kuwa ngome isiopitika tena. (Star)

Danny Rose anategemewa kuanza na kikosi ch akwanza cha Tottenham kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund Jumanee hii.

Klabu ya Borussia Dortmund inasistiza kwamba, Michael Zorc hataungana na Sven Mislintat Arsenal.

Mesut Ozil anatarajiwa kufanya uamuzi utakaoibu hisia za wengi kwa kurejea kwenye klabu yake ya nyumbani, Schalke 04.

Willian amekanusha taarifa zote zilizokuwa zinadai ana mpango wa kurejea Brazil hivi karibuni.

Kenwyne Jones
Aliyekuwa mshambuliaji wa Sunderland na Stoke City, Kenwyne Jones amesema kwamba, mwaka huu ndio mwisho kwake kucheza soka. (Sun)

Manchester United wamepitia upya mkataba wa Ander Herrera na sasa nyota huyo amezuiliwa Old Trafford hadi mwaka 2019. (Daily mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 21 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 21 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/21/2017 10:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.