Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Novemba, 2017

Pierre-Emerick Aubameyang
Klabu ya Chelsea imepewa nafasi ya kumsajili nyota wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang mwezi Januari.

Borussia Dortmund wana mpango wa kumsajili nyota wa Manchester United, Angel Gomes mwezi Januari.

Mark Hughes anasistiza kwamba, Xherdan Shaqiri hataondoka Stoke City mwezi Januari.

Jose Mourinho amewaacha Luke Shaw, Marouane Fellaini na Henrikh Mkhitaryan nje ya kikosi kitakachoivaa Watford.

Jean Michael Seri
Arsenal watakutana na ushindani mkubwa kutoka klabu ya Barcelona kwenye kusaka saini ya kiungo wa Nice, Jean Michael Seri. (Mirror)

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anataka kusajili mabeki wapya wa kulia na kushoto katika kipindi cha madirisha mawili ya usajili yajayo.

Klabu ya Barcelona iko tayari kushdindana na Borussia Dortmund kusaka saini ya nyota wa Manchester United, Angel Gomes.

Alan Pardew anatarajiwa kutangazwa kama meneja mpya wa West Brom ndani ya masaa 24 yajayo. (Sun)

Klabu ya Stoke City inatarajia kuwauza nyota wake, Glenn Johnson na Charlie Adam katika dirisha dogo la usajili Januari. (Telegraph)

Raul Sanllehi
Arsenal wanakaribia kumchukua aliyekuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Barcelona, Raul Sanllehi baada ya kujiuzulu cheo chake Nou Camp.

Nyota wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha anasema kuwa anaichukia sana Brighton.

uwezekano wa Mesut Ozil kuikosa mechi ya Arsenal dhidi ya Huddersfield ni mkubwa sana.

Tottenham wanmfuatilia nyota wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon kwa ajili ya kujaza nafasi itakayoachwa na Danny Rose.

Rafa Benitez amewaonya mashabiki wa Newcastle kwamba msimu huu unaweza kuwa mbaya zaidi kwao.

Eden Hazard na Tiemoue Bakayoko walijumuishwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichoelekea nchini Ufaransa, licha ya kulalamikia ugumu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Uingereza. (Daily Mail)

Ruben Loftus-Cheek
Ruben Loftus-Cheek anasema kwamba, Wilfried Zaha amekuwa akimwelezea kuhusu upinzani wa klabu ya Crystal Palace na Brighton. (Express)

David Moyes amemhimiza David Unsworth kuondoka Everton kama aakosa nafasi ya kuwa meneja wa klabu hiyo. (Star)

Alan Pardew ameomba apewe mkataba wa miaka mitatu ili akubali kuchukuwa kibaru cha kuinoa klabu ya West Brom kwa miaka mitatu. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 28 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/28/2017 04:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.