Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 5 Novemba, 2017

Hatem Ben Arfa
Hatem Ben Arfa anatarajiwa kurejea Ligi Kuu ya Uingereza aungane na Meneja wake wa zamani, Claude Puel katika klabu ya Leicester City. (Sun)

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anapigana kulinda kibarua chake.

Miliki wa klabu ya Chelsea, Roma Abramovich amenunua jengo la nne lenye thamani ya dola za marekani milioni 96 upande wa magharibi ya juu ya mji.

Dele Alli na Harry Winks wakishangilia bao
Klabu za Barcelona na Real Madrid zaingia vitani kusaka huduma ya nyota wa klabu ya Tottenham, Dele Alli na Harry Winks.

Beki wa PSG, Dani Alves amekiri kwamba uamuzi wa kuhamia Juventus kutokea Barcelona ulikua mbaya sana katika maisha yake ya soka. (Daily Mail)

Meneja wa Watford, Marco Silva yuko msatari wa mbele kati ya mameneja wanaowaniwa na klabu ya Everton.

Meneja wa Cystal Palace, Roy Hodgson anadai Dele Alli anahitajiwa na klabu nyingi kubwa za Ulaya.(Star)

Juan Mata anadai Romelu Lukaku atakuja kuwa kama mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba.

Jose Mourinho anataka ongezeko kubwa kwenye mshahara wake ili kusaini mkataba mpya kama meneja wa Manchester United.

Alexis Sanchez anatarajiwa kuwa kivutio kwa klabu nyingi barani Ulaya
Rais wa PSG anaamini Alexis Sanchez tayari ameshachagua klabu atakayojiunga nayo mwezi Januari.

Everton wamepandisha dau kwa lengo la kumnasa meneja Sean Dyche ajaze nafasi iliyoachwa na Koeman.

Leon Goretzka
Arsenal yakutana na ushindani mkubwa kutoka kwa Tottenham katika kuiwinda saini ya Leon Goretzka.

Fernandinho anatarijwa kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Manchester City hivi karibuni. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 5 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 5 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/05/2017 10:06:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.