Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 19 Novemba, 2017

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry
Thierry Henry yuko miongoni mwa waliotajwa kwenye orodha ya makocha wanatarajiwa kuchukua nafasi ya Chris Coleman Wales.

Manchester United wako tayari kumpa ofa Danny Rose itakayomfanya aachane na klabu ya Tottenham.

Mbrazil, Ronaldinho Gaucho anaamini Philippe Coutinho atapata mafanikio makubwa akihamia Barcelona.

Jose Mourinho ataigharimu klabu ya Paris Saint-Germain kiasi cha paundi milioni 30 kama itamuhitaji katika kipindi cha majira ya joto.

Manchester United wanatarajia kupokea ofa nyingine kutoka klabu ya Real Madrid kwa ajili ya kumnasa David de Gea.

Klabu ya West Brom inamtaka Michael O'Neill kama itamfukuza kazi meneja wao wa sasa, Tony Pulis.

Arsenal wana mpango wa kuwavuta Emirates, mkurugenzi wa michezo, Michael Zorc na Sven Mislintat kutoka klabu ya Borussia Dortmund.

Liverpool iko tayari kuingia vitani dhidi ya klabu za Chelsea na Arsenal kuwania saini ya Bernad
Liverpool wanashindana na klabu za Chelsea na Arsenal kumsajili winga wa Brazil, Bernard anayeichezea Shakhtar Donetsk. (Mirror)

Gianluigi Buffon bado anapigania kurejea kwenye hali yake ya kawaida baada ya Timu yake ya Taifa kushindwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia na hatakuwemo kwenye kikosi cha Juventus kitakachocheza dhidi ya Sampdoria Jumapili hii.

Paris Saint-Germain watalazimika kulipa paundi milioni 20 kama fedha za fidia kwa Jose Mourinho kama watataka kumsajili kocha huyo wa Manchester United katika majira ya joto.

Danny Rose
Mauricio Pochettino anasistiza kwamba, suala la kumwacha Danny Rose nje ya kikosi kilichocheza na Arsenal ilitokana na hali yake kutokuwa fit kutokana na kuwa nje kwa muda wa miezi tisa. (Daily Mail)

Jose Mourinho yuko tayari kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota wa klabu ya Chelsea, Willian kama ataondoka Stamford Bridge mwezi januari.

Klabu ya Real Madrid ina mpango wa kumsajili nyota wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann kama Gareth Bale atapata mnunuzi. (Express)

Manchester City watamwachia Joe Hart ambaye anaichezea klabu ya Westham kwa mkopo hivi sasa aondoke moja kwa moja kwa kiasi cha fedha kati ya paundi milioni 3 na 6 katika majira ya joto. (Star)

Patrick van Aanholt ni miongoni mwa wachezaji walioko kwenye orodha ya wachezaji muhimu anaowataka meneja wa Manchester City, Pep Guardiola.

West Ham watampa David Moyes kiasi cha paundi milioni 30 katika vita ya usajili mwezi Januari kwa ajili ya kumsajili William Carvalho na Hazam Barry.

Everton watatoa ofa ya paundi milioni 12 kumnasa meneja wa klabu ya Watford, Marco Silva.

Richarlison
Chelsea wako tayari kuingia vitani na Tottenham kuwania saini ya winga wa klabu ya Watford, Richarlison.

Liverpool wako hatari kumpoteza mshindi wa kombe la dunia chini ya U17, Rhian Brewster ambapo mshambuliaji huyo anaweza kumfuata Jadon Sancho katika klabu ya Borussia Dortmund. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 19 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 19 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/19/2017 02:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.