Texas: Watu 26 wauawa kwa kupigwa risasi wakiwa kanisani
Wakazi walihudhuria mkesha wa kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio hilo la Sutherland Springs |
Shambulio hilo lilitekelezwa katika kanisa la First Baptist Church katika mji wa Sutherland Springs, mji mdogo katika wilaya ya Wilson, Texas.
Mshambuliaji, ambaye anadaiwa kuuawa baada ya kutekeleza mauaji hayo, aliingia kanisani na kuanza kuwafyatulia risasi watu mwendo wa saa tano na nusu asubuhi.
Gavana Greg Abbott amethibitisha idadi ya waliofariki na kusema ndicho kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya texas.
Mkuu wa idara ya usalama wa Texas Freeman Martin amesema waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 5 na 72.
Maafisa wamesema watu zaidi ya 20 pia walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini.
Martin amesema mshukiwa ni mwanamume mzungu wa umri wa miaka 20 ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi na fulana ya kujikinga dhidi ya risasi pamoja na kuwa na bunduki yenye uwezo mkubwa.
Alianza kufyatua risasi akiwa nje ya kanisa kabla ya kuingia ndani na kuendelea kufyatulia watu risasi.

"Kutakuwa na majonzi na masikitiko makubwa kwa wale walioathiriwa," aliwaambia wanahabari.
Mkuu wa idara ya usalama wa Texas Freeman Martin amesema waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 5 na 72.
Maafisa wamesema watu zaidi ya 20 pia walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini.
Martin amesema mshukiwa ni mwanamume mzungu wa umri wa miaka 20 ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi na fulana ya kujikinga dhidi ya risasi pamoja na kuwa na bunduki yenye uwezo mkubwa.
Alianza kufyatua risasi akiwa nje ya kanisa kabla ya kuingia ndani na kuendelea kufyatulia watu risasi.
Mwenyeji "alitwaa bunduki yake na kuanza kumfyatulia " risasi mshukiwa kabla ya mshukiwa huyo kutoroka akitumia gari.
Polisi walimpata mshukiwa akiwa amefariki ndani ya gari lake.
Haijabainika iwapo alifariki kutokana na majeraha ya risasi aliyojisababishia mwenyewe au kutokana na mejaraha yaliyosababishwa na raia huyo, aliongeza Martin.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari Marekani, mshukiwa alitambulika kwa jina la Devin P Kelley, 26, lakini polisi bado hawajathibitisha jina lake.
Mhubiri wa kanisa hilo la First Baptist Frank Pomeroy, ameambia ABC News kwamba binti yake mwenye umri wa miaka 14, kwa jina Annabelle ni miongoni mwa waliouawa katika shambulizi hilo.
Sutherland Springs ni mtaa mdogo wenye wakazi wasiozidi elfu moja ambao hupatikana takribani kilomita 50 hivi kusini mashariki mwa mji wa San Antonio mjini Texas.
Maafisa wa FBI kutoka San Antonio wametumwa kufanya uchunguzi lakini hadi kufika hivi sasa lengo la mshambuliaji halijabainika.
FBI pia wamesema mshambuliaji alikuwa mmoja pekee, lakini bado wanachunguza uwezekano wa iwapo kuna mtu mwingine aliyehusika.
Rais Donald Trump, ambaye yumo ziarani Asia, ameshutumu kisa hicho na kusema ni "kitendo cha uovu" na kusema kwamba Wamarekani watajikwamua na kusalia na umoja.

"Na kupitia kwa machozi na kupitia huzuni hii, tunasalia imara, imara zaidi," ameongeza.
May God be w/ the people of Sutherland Springs, Texas. The FBI & law enforcement are on the scene. I am monitoring the situation from Japan.— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) November 5, 2017
Mauaji hayo yametokea mwezi mmoja tu baada ya mshambuliaji mwingine kufyatulia risasi watu waliokuwa wakihudhuria tamasha ya muziki Las Vegas na kuwaua watu 58 pamoja na kujeruhi mamia wengine, katika kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutumia bunduki katika historia ya Marekani nyakati za karibuni.
Texas: Watu 26 wauawa kwa kupigwa risasi wakiwa kanisani
Reviewed by Zero Degree
on
11/06/2017 01:17:00 PM
Rating: