Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Januari, 2018

Frank Lampard
Frank Lampard amekanusha kufanya mazungumzo na klabu ya Oxford United juu ya kazi ya ukufunzi.

Inter Milan inaweza kujaribu kumsajili winga wa klabu ya Tottenham, Eric Lamela kwenye majira ya joto. 

Klabu ya West Ham imethibitisha kukamilisha uhamisho wa Joao Mario kutoka Inter Milan kwa mkopo. (Sky Sports)

Paris Saint-Germain imesisitiza kwamba haitawezekana kwa Real Madrid kufanikiwa kuipata saini ya Neymar katika majira ya joto mwaka huu kitu ambacho kitaiongezea hofu klabu ya Chelsea kwani Mabingwa wa UEFA wanaweza kugeukia kwa Eden Hazard.

Tottenham wamemtembeza Lucas Moura kwenye uwanja wao wa mazoezi, huku wakiwa tayari kutoa ofa ya kumnasa nyota huyo kutoka Paris Saint-Germain kabla dirisha la usajili halijafungwa wiki ijayo. (Telegraph)

Sergio Ramos anasema kuwa bado ana imani na Zinedine Zidane, licha ya klabu ya Real Madrid kuwa na hali mbaya msimu huu.

Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amechukizwa na Antonio Conte, baada ya Muitaliano huyo kudai kwamba hakuhusika kwenye usajili uliofanywa msimu huu.

Javi Gracia amekiri kuwa haelewi atakuwa meneja wa klabu ya Watford kwa muda gani.

Pierre-Emerick Aubameyang
Arsenal imeambiwa na Borussia Dortmund kuwa inatakiwa kuvunja rekodi yao ya usajili ili kufanikiwa kumnasa Pierre-Emerick Aubameyang.

Nyota wa klabu ya Everton anayewindwa na Newcastle, Sandro Ramirez ameiambia klabu yake kuwa anataka kuhamia Sevilla. (Star)

Liverpool imeipiku Manchester United kwa kufanikisha uhamisho wa chipukizi wa klabu ya Falkirk, Tony Gallacher.


Watford wemefanya uchunguzi juu ya uwezekano wa uhamisho wa Loic Remy kwa mkopo kutoka Las Palmas.

Stoke City bado hawajakubaliana na klabu ya MLS kuhusu ada ya uhamisho wa Jack Harrison.

Sevilla inakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Swansea, Roque Mesa kwa mkopo.

Brighton inajidili uhamisho wa Victor Camarasa wa Real Betis pamoja na Ezri Konsa wa Charlton.

Manchester City inatazamia kumsajili chipukizi wa klabu ya PSG, Claudio Gomes. (Daily Mail) 


James Maddison
West Ham imetoa ofa ya pauni milioni 12 kumnasa kiungo wa klabu ya Norwich na timu ya taifa ya Uingereza, James Maddison. (Guardian) 

Aston Villa inamfukuzia mshambuliaji wa Leicester, Leonardo Ulloa, ambaye ataruhusiwa kuondoka endapo tu, Islam Slimani atauzwa. (Times) 

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino hajapinga na tetesi zinazodai anaweza kwenda kuinoa Real Madrid, lakini anasema kuwa ni bora kufanya kazi za shamba kuliko kuwa mkufunzi wa Arsenal au Barcelona. (Express) 

Borussia Dortmund imetoa ofa ya pauni milioni 1.3 kwa Arsenal kumnasa Olivier Giroud kwa mkopo katika kipindi cha msimu huu kilichosalia, kitu ambacho kinaweza kutibua mipango ya Arsene Wenger kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang.

Newcastle ina matumaini ya kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kumnasa  Nicolai Jorgensen kutoka Feyenoord kwa dau la pauni milioni 18 ndani ya masaa 48 yajayo.

Meneja wa klabu ya Watford, Javi Gracia amekiri kwamba hana uhakika kama Troy Deeney atabaki katika klabu hiyo mwezi huu.

West Ham inafikiria kupeleka ofa mezani kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge kwa mkopo.

Diafra Sakho
Diafra Sakho ameambia West Ham kuwa anataka kuondoka aende kujiunga na klabu ya Rennes ya Ufaransa.

Stoke City inaonekana kuwa na lengo la kuachana na mpango wa kumrejesha Bojan kutoka klabu ya Alaves alikokuwa kwa mkopo. 

Arsenal inajiandaa kumsajili kiungo wa klabu ya Corinthians na timu ya taifa ya Brazil, Maycon, 20. 

Brighton inafanya mpango wa kumsajili beki matata wa klabu ya Charlton, Ezri Konsa. (Sun) 

Manchester City inatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte wikendi hii. 

Chelsea inafikiria juu ya uhamisho wa Olivier Giroud kutoka Arsenal.

Meneja wa Henrikh Mkhitaryan katika timu yake ya taifa ya Armenia amempongeza nyota wake kwa kufanikiwa kuachana na meneja wa Manchester United Jose Mourinho na kujiunga na klabu ya Arsenal.

Nyota wa Liverpool, Danny Ings anayewindwa na Inter Milan, anategemewa kuanza na kikosi cha kwanza chini ya uongozi wa Jurgen Klopp baada ya kusubuliwa na majeruhi kwa karibuni miaka miwili.

Winga wa klabu ya Bournemouth, Connor Mahoney anatarajiwa kujiunga na Barnsley kwa mkopo. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/26/2018 09:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.