Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 30 Januari, 2018

Thomas Lemar
Makamu wa rais wa klabu ya Monaco, Vadim Vasilyev amesema kuwa Thomas Lemar ataendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu.


Klabu ya Stoke City imekubali kulipa ada ya pauni milioni 15 kwa ajili ya uhamisho wa kiungo wa klabu hiyo ya Uturuki, Badou Ndiaye. 

Arsenal imefikia makubaliano na Borussia Dortmund juu ya uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang, lakini klabu hiyo ya Ujerumani haiko tayari kumruhusu aondoke hadi itakapopata mchezaji wa kuchukua nafasi yake.

Charly Musonda: Ilichukua muda mfupi sana kuamua kujiunga na klabu ya Celtic kwa mkopo. (Sky Sports)

Chelsea haitakubali kupokea ofa ya Manchester City kwa ajili ya uhamisho wa Eden Hazard - hata kama vinara hao wa Ligi Kuu ya Uingereza watavunja rekodi ya dunia kwa kutoa dau la zaidi ya pauni milioni 200.

Klabu ya Chelsea ina matumaini ya kumnasa Olivier Giroud, usajili huo ndio utakaokamilisha dili la uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang kwenda Arsenal na Michy Batshuayi kwenda Borussia Dortmund. (Telegraph)

Arsenal, Borussia Dortmund na Chelsea zinahusika katika uhamisho wa wachezaji watatu, ambao ni Aubameyang, Giroud na Batshuayi.

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge amaejunga na West Brom kwa mkopo. (talkSport)

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa klabu yake haimhitaji Aubameyang.

Winga wa klabu ya Chelsea Charly Musonda amejiunga na Celtic kwa mkopo na kusaini mkataba wa miezi 18.

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang
Uhamisho wa Aubameyang kwenda Arsenal ltafanikiwa endapo tu klabu hiyo ya Ujerumani itapata mchezaji atakayechukua nafasi yake. (ESPN)  

Borussia Dortmund inatarajia kumnasa nyota wa klabu ya Chelsea, Michy Batshuayi achukue nafasi ya Pierre-Emerick Aubameyang.

Arsenal inaweza isifanikiwe kukamilisha dili la uhamisho wa Jonny Evans baada ya West Brom kuonyesha nia ya kutaka kumbakisha beki huyo kikosini hadi kwenye majira ya joto. (Times)

Newcastle United ilikuwa na matumaini ya kumnunua Daniel Sturridge baada ya kumalizika kwa msimu huu kabla nyota huyo hajaamua kujiunga na West Brom.

Newcastle inamtaka beki wa klabu ya Manchester City, Eliaquim Mangala kwa mkopo.

Manchester City inatarajiwa kumsajili Jack Harrison kutoka New York City na kumpeleka katika klabu ya Middlesbrough kwa mkopo.

Klabu ya Juventus ina matumaini ya kufanikiwa kumnasa kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya Ujerumani, Emre Can kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu, ambapo mkataba wake utakuwa umeisha.

Manchester City imekubali kulipa pauni milioni 2.6 kwa ajili ya uhamisho wa chipukizi wa klabu ya PEC Zwollo, Philippe Sandler.
Watford imekataa ofa ya klabu ya Malaga kumsajili Isaac Success kwa mkopo.

Klabu ya Swansea inafanya mpango wa kumsajili winga kutoka Liverpool, Lazar Markovic kwa mkopo.

Pep Guardiola atafikisha kiasi cha pauni milioni 450 kwenye matumizi yake katika klabu ya Manchester City atakapokamilisha usajili wa Aymeric Laporte kutoka Athletic Bilbao. (Daily Mail)

Klabu ya Motherwell imekataa ofa ya pauni 200,000 kutoka Celtic kwa ajili ya uhamisho wa golikipa wao, Trevor Carson. (Record)

Fernando Llorente
Chelsea imemrejesha Fernando Llorente kwenye mipango yao ya usajili - kama itashindwa kumnasa Giroud.

Roy Hodgson ametoa ofa kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wa Norway, Alexander Sorloth.

Meneja wa Burnley, Sean Dyche ameikataa ofa ya pauni milioni 10 kutoka klabu ya Nottingham Forest kwa ajili ya uhamisho wa Joe Worrall. (Sun)

Aston Villa ina matamanio makubwa ya kumsajili nyota wa klabu ya Dynamo Dresden, Haris Duljevic.

Arsene Wenger anaweza kulazimika kumwacha Olivier Giroud ajiunge na klabu ya Chelsea ili afanikiwe kukamilisha dili la uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.


Aliyekuwa kiungo wa Manchester United, David Beckham ameshangazwa na uamuzi wa klabu ya Arsenal kumuuza Alexis Sanchez.

Sam Allardyce amemwambia Davy Klaassen, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25, kuwa anatakiwa aondoke kwa mkopo ili apate nafasi ya kurejea katika nafasi yake kwenye kikosi cha Everton. (Mirror)
West Ham ina matumaini ya kufaniwa kumsajili Morgan Schneirderlin kutoka klabu ya Everton na nahodha wa Urusi, Fedor Smolov kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Jumatano.

Stoke City inakaribia kukamilisha uhamisho wa kiungo wa klabu ya Galatasaray, Badou Ndiaye kwa pauni milioni 15.

Klabu ya Southampton imekanusha kuwa na mpango wa kummuza Manolo Gabbiadini kwenda Bologna.

David Luiz
Beki wa klabu ya Chelsea, David Luiz ametolewa kama ofa kwa Arsenal kufanikisha uhamisho wa Olivier Giroud. (Star)


Watford inahitaji pauni milioni 20 ili kumwachia nyota wao Troy Deeney ajiunge na klabu ya West Brom. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 30 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 30 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/30/2018 04:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.