Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 14 Januari, 2018
Neymar |
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane hakubaliani na ombi la Neymar kwa rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, baada ya nyota huyo kutaka awe mchezaji pekee ambaye nafasi yake dimbani haitaguswa na kuwa mchezaji atakayelipwa mshahara mkubwa kuliko wote. (Don Balon)
Manchester United wamejiandaa kumfanya Alexis Sanchez kuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza kulipwa pauni 350,000 kwa siki.
Arsenal inawania saini ya Malcom, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 35.
Klabu ya Manchester City inamvizia kuingo wa Lille, Boubakary Soumare.
Golikipa wa Getafe, Vicente Guaita anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Roy Hodgson kama meneja wa Crystal Palace kwa dau la pauni milioni 3.5m. (Daily Mail)
Henrikh Mkhitaryan |
Jose Mourinho amefungua milango kwa Henrikh Mkhitaryan kama atahitaji kuondoka katoka klabu hiyo.
Liverpool wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez. (ESPN)
West Ham inafuatilia mstakabali wa mkataba wa Marouane Fellaini katika klabu ya Manchester United.
West Ham inafuatilia mstakabali wa mkataba wa Marouane Fellaini katika klabu ya Manchester United.
Stoke City watamtangaza Martin O'Neill kuwa meneja wao mpya ndani ya masaa 48 yajayo. (Star)
Alexis Sanchez ataingiza pauni 60,000 za ziada kwa wiki Manchester United kama ataichagua klabu hiyo dhidid ya Manchester City mwezi huu.
Fulham inafuatilia mshambuliaji Nelson Oliveira wa Norwich baada ya klabu ya Derby kuweka ofa ya pauni milioni 8 mezani. (Sun)
Alex Sandro |
Mourinho yuko tayari kushindana na Antonio Conte - wakati huu ikiwa ni katika vita ya kuwania saini ya beki wa klabu ya Juventus, Alex Sandro.
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amemalizana na uongozi wa klabu hiyo baada ya mkurugenzi msaidizi, Ed Woodward kuahidi kutoa pauni milioni 120 kufanikisha uhamisho wa Alexis Sanchez.
Meneja wa klabu ya West Ham, David Moyes ataijaribu klabu ya Everton kwa kutoa ofa ya kumnasa kiungo wa klabu hiyo, Tom Davies.
Stoke City wanasubiria uamuzi wa Martin O'Neill's juu ya kazi ya umeneja katika klabu hiyo.
Liverpool bao wako kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Schalke, Leon Goretzka. (Mirror)
Manchester United wamempa mshambuliaji wa Arsena, Alexis Sanchez siku ya Ijumaa kuwa tarehe ya mwisho kukamilisha taratibu za uhamisho zaidi ya hapo wataachana naye. (Express)
Alexis Sanchez |
Stoke City wamewapa Martin O'Neill na Roy Keane ofa za kurejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 14 Januari, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
1/14/2018 01:53:00 PM
Rating: