Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 15 Januari, 2018
Ryan Giggs |
Ryan Giggs ameteuliwa kuwa meneja mpya wa Timu ya Taifa ya Wales kuchukuwa nafasi iliyoachwa na Chris Coleman.
Klabu ya Sunderland imekubali kuvunja mkataba wa Jack Rodwell, baada ya nyota huyo anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika klabu hiyo kuomba kuondoka.
Newcatle wameshindwa kamilisha dili la kumsajili kwa mkopo golikipa wa Sparta Prague, Martin Dubravka. (Sky Sports)
Arsenal ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa klabu ya Bordeaux, Malcom siku ya Jumapili na inatarajia kulipa dau la pauni milioni 40 kumnasa Mbrazil mwenye umri wa miaka 20.
Arsenal na Chelsea wana matamanio makubwa ya kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Watford raia wa Brazil, Richarlison.
Antonio Conte hajazungumza lolote kuhusu kuwa na mpango wa kurejea Italia kwa mara ya pili kama meneja wa timu ya taifa hilo endapo ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu. (Express)
Bournemouth inatarajiwa kuipiku Celtic na kumnasa chipukizi wa klabu ya Chelsea, Charly Musonda.
Crystal Palace watatakiwa kulipa pauni milioni 15 ili kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Fiorentina, Khouma Babacar. (Guardian)
Sam Allardyce hatamhakikishia Theo Walcott nafasi ya kuwa mshambuliaji wa kati wa kudumu ikiwa atafanikiwa kumsajili nyota huyo kutoka Arsenal mwezi huu.
Sam Allardyce hatamhakikishia Theo Walcott nafasi ya kuwa mshambuliaji wa kati wa kudumu ikiwa atafanikiwa kumsajili nyota huyo kutoka Arsenal mwezi huu.
Klabu nyingi za ulaya zilipewa ofa ya kumsajili Mohamed Salah kwa pauni milioni 2.5, lakini Hull City na Stoke City pekee ndio zilionyesha nia ya kumtaka nyota huyo ambaye kwa sasa anakipiga Liverpool.
Mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa, Scott Hogan |
Scott Hogan amemwambia Steve Bruce asihangaishe kununua straika mwingine mwezi huu kwa sababu anaamini kwamba, anaweza kuyabeba majukumu hayo katika klabu ya Aston Villa. (Daily Mail)
Manchester United wanaamini wako kwenye nafasi ya kufanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez baada ya kumfuatilia kimya kimya kwa muda wa miezi 8. (Star)
Alexis Sanchez anakaribia kujiunga na Manchester United, huku Arsenal ikiwa na nia ya kumsajili Henrikh Mkhitaryan kama sehemu ya makubaliano yao na wakati huo huo wakifuatilia uwezekano wa kumnasa nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.

Martin O'Neill aliachana na dili la kuinoa Stoke kwa sababu hakutaka kuvunja agano lake na shirikisho la soka la Ireland wakati alipopewa ofa ya mkataba mpya mwezi Octoba.
Uamuzi wa O'Neill's kuipotezea Stoke City inamaanisha kwamba klabu hiyo inaweza kugeuzia nguvu yao kwa aliyekuwa meneja wa klabu ya Aston Villa, Paul Lambert. (Telegraph)
Paris Saint-Germain inaripotiwa kuwa kwenye mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Chelsea, N'Golo Kante kwenye majira ya joto.
N'Golo Kante |
Swansea inafanya mpango wa kuvunja rekodi kwa kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Kevin Gameiro kwa pauni milioni 25, ambaye anawindwa na klabu ya Fenerbahce pia.
Schalke 04 wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo beki wa klabu ya Chelsea, Baba Rahman kwa mara ya pili.
Newcastle wanakaribia kukamilisha usajili wa mkopo wa beki wa Crystal Palace, Pape Souare kwa kipindi chote kilichosalia kabla ya msimu huu haujamalizika.
Ipswich wameanza mazungumzo na Crystal Palace juu ya uhamisho wa golikipa wao, Bartosz Bialkowski kwa pauni milioni 4. (Sun)
Liverpool wameachana na mpango wa kumsajili winga wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar baada klabu hiyo ya Ufaransa kutaka dau la pauni milioni 90 ili kumwachia nyota huyo. (Times)
Manchester United watampa David de Gea ofa ya mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki ili abakie Old Traford katika kipindi chote cha maisha yake ya soka kilichobaki.
Bayern Munich inatarajiwa kumnasa raia wa Ujerumani, Leon Goretzka, ambaye anaichezea Shalke 04 mbele ya Liverpool na Arsenal
Chris Hughton amepewa ahadi ya kitita mwezi Januari ili aongeze mshambuliaji mwenye kiwango cha juu kwenye kikosi chake.
Timothy Fosu-Mensah |
Jose Mourinho ataoa uamuzi wake wa mwisho juu ya future ya Timothy Fosu-Mensah katika klabu ya Manchester United.
Tottenham ina imani ya kuibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya chipukizi wa klabu ya Stevenage, Ben Wilmot.
Watford, Crystal Palace na Stoke City zote zina nia ya kumsajili kiungo wa klabu ya Galatasaray, Badou Ndiaye. (Mirror)
Antonio Conte hajazungumza lolote kuhusu kuwa na mpango wa kurejea Italia kwa mara ya pili kama meneja wa timu ya taifa hilo endapo ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu. (Express)
Bournemouth inatarajiwa kuipiku Celtic na kumnasa chipukizi wa klabu ya Chelsea, Charly Musonda.
Ikiwa klabu ya Celtic itashindwa kumnasa Musonda, itahamishia nguvu zake kwa mshambukiaji wa Schalke o4, Franco Di Santo. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 15 Januari, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
1/15/2018 06:26:00 PM
Rating: