Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 29 Januari, 2018

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo anaweza kurejea katika Ligi Kuu ya Uingereza, safari hii ikiwa ni katika klabu ya Chelsea na sio Manchester United. (ESPN)

Kuchelewa kwa dili la uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang kunamaanisha Arsenal watamruhusu Olivier Giroud ajiunge na klabu ya Chelsea kama majirani zao watakubali kulipa dau la pauni milioni 35.

West Bromwich Albion wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 18 kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wa Watford, Troy Deeney.

Arsenal inasita kumruhusu beki wake, Rob Holding aondoke kwa mkopo kufuatia ombi lililotolewa na klabu ya Burnley. (Daily Mail)

Arsenal inakaribia kukubali kulipa ada ya karibu pauni milioni 60 kwa ajili ya uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Dortmund.

West Ham iko kwenye mazungumzo na aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Southampton, Graziano Pelle anayeichezea Shandong Luneng ya China.

Meneja wa klabu ya Barcelona, Victor Valverde ana mpango wa kusajili beki mwingine.

Kwa mujibu wa Gerlad Pique, beki wa klabu ya Real Madrid anataka klabu yake imsajili beki wa Real Sociedad, Ingo Martinez. (Don Balon)

Newcastle imeongeza ofa yake kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Feyenoord, Nicolai Jorgensen lakini haijafikia kiasi ambacho kinahitajika. (Times)

Toomy Elphick anatarajiwa kujiunga na klabu ya Reading kwa mkopo akitokea Aston Villa. (Sky Sports)

Antonio Conte 
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amesema kwamba anataka kumbakisha mshambuliaji wake, Michy Batshuayi katika klabu hiyo hadi kwenye majira ya joto.

Klabu ya Stoke City italazimika kulipia pauni milioni 16 kumnasa nyota wa klabu ya Galatasaray, Badou Ndiaye.

Swansea ina matumaini ya kufanikiwa kukamilisha dili la kumrejesha Andre Ayew kutoka West Ham, uhamisho utakaogharimu pauni milioni 18. (Sun)

Asernal inakaribia kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kumnasa mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyanga.

Joey Burton amemwambia Pep Guardiola aachane na kulalamikia waamuzi, badala yake azoee mfumo wa Ligi Kuu ya Uingereza. (talkSport)

Edin Dzeko
Dili la uhamisho wa mshambuliaji wa klabu ya Roma, Edin Dzeko kwenda Chelsea liko hatarini kukwama baada ya klabu hizo mbili kushindwa kufikia makubaliano hadi sasa. (Independent)

Manchester United imeinga kwenye mbio za kuwania saini ya Arturo Vidal, huku klabu ya Bayern Munich ikionekana kuwa tayari kumuuza kiungo huyo.
 (Mirror)

Manchester City, Real Madrid na Barcelona zote zina nia ya kumsajili beki wa klabu ya Inter Milan na timu ya taifa ya Slovakia, Milan Skriniar.

Klabu ya Arsenal ina matamanio makubwa ya kuipata saini ya beki wa klabu ya West Brom, Jonny Evans - na inaamini kuwa inaweza kumnasa nyota huyo kwa bei nafuu. (Star)

Charly Musonda
Nyota wa klabu ya Chelsea, Charly Musonda anatarajiwa kutua mjini Glasgow hapo kesho, kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Celtic. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 29 Januari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 29 Januari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 1/29/2018 01:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.