Loading...

Magari 120 ya wagonjwa kusambazwa katika vituo vya afya nchi nzima


SERIKALI imesema itasambaza magari 120 ya wagonjwa yenye thamani ya Sh bilioni 10 katika vituo vya afya nchi nzima, ikiwa ni nyongeza kwa magari mengine 70 ambayo yalishasambazwa hivi karibuni katika vituo kadhaa vya afya.

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Kahangara, wilaya ya Magu jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema serikali imeamua kuhakikisha inakabiliana na upungufu uliopo katika sekta mbalimbali, ikiwemo ya afya na kwamba itahakikisha wananchi wanafikiwa na huduma zenye kiwango.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, ni lengo la serikali kuona huduma muhimu zinaboreshwa kwa wakati na kuongeza kuwa afya ni miongoni mwa maeneo yanayohitaji ufadhili wa kutosha ili kuwa na ubora unaotakiwa.

"Hivi sasa tunajenga vituo vingi vingine vya afya vikiwemo ambavyo tutaweka mahitaji muhimu yakiwemo magari ya wagonjwa. Karibu tutaongeza magari ya wagonjwa 120, ili kuhakikisha vituo vya afya vinakuwa vimejidhatiti,” alisema. 

Waziri Mkuu alipongeza Wilaya ya Magu kwa kujenga kituo cha afya cha Kahangara, ambacho kwa mujibu wake ni moja ya kituo cha kisasa kilichotengenezwa kulingana na thamani ya fedha.

Alisema ili kutoa huduma za viwango, usambazaji wa dawa utapewa kipaumbele na kuongeza kuwa Wilaya ya Magu imetengewa Sh milioni 498 na kuzitaka mamlaka za ndani kutumia fedha hizo vizuri.

Aliongeza vituo vya afya sio tu vitajengwa lakini pia vitawekewa vifaa na uhuduma muhimu na kuwa Kahangara itapewa Sh milioni 200 kwa ajili ya kuweka vifaa vitakavyowezesha kufanya operesheni ndogo.

Waziri Mkuu alivitahadharisha vituo vya afya kutonunua dawa zisizohitajika na kuvitaka kuagiza dawa kulingana na mahitaji na si vinginevyo.

Katika kupunguza mzigo wa gharama za tiba, Waziri Mkuu aliwashauri wakazi wa Magu wanajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambayo gharama yake kujiandikisha sasa ni Sh 10,000 kwa familia na kufurahia matibabu.
Magari 120 ya wagonjwa kusambazwa katika vituo vya afya nchi nzima Magari 120 ya wagonjwa kusambazwa katika vituo vya afya nchi nzima Reviewed by Zero Degree on 2/18/2018 11:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.