Loading...

Maofisa wapya wa JWTZ watunukiwa kamisheni

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya 192 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pamoja na Maafisa kadhaa kutoka nchi marafiki katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam
RAIS John Magufuli amewatunuku kamisheni maofisa wapya 197 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliomaliza mafunzo katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli mkoani Arusha.

Sherehe hiyo ya kutunuku kamisheni kwa maofisa wa kundi la 62 ilifanyika jana Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Tafa, Dk Hussein Mwinyi, makatibu wakuu na manaibu, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa taasisi, mawaziri na viongozi wengine mbalimbali.

Kati ya maofisa hao, watatu ni kutoka nchi rafiki ambao walipata mafunzo hapa nchini katika chuo hicho. Aidha, kati ya maofisa hao 197, 169 ni wanaume ambapo 11 ni kutoka nchi rafiki wa Tanzania.

Pia maofisa 28 ni wanawake ambapo ni kutoka Tanzania na wengine kutoka nchi rafiki ambazo ni Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda. Maofisa tisa ni wale Watanzania waliopata mafunzo nje ya nchi ambapo wane walipata mafunzo Burundi, watatu Uingereza, mmoja China na watatu Kenya.

Kabla yatunuku kamisheni, Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu alikagua gwaride akisindikizwa na Mkuu wa Chuo cha Monduli, Paul Massao na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo.

Pia Rais alitoa zawadi kwa wanafunzi hao waliofanya vizuri katika kipindi cha mafunzo hayo ambapo aliyefanya vizuri zaidi alitajwa kuwa ni Michael Igoti na katika waliofanya vizuri darasani ni Sambulufu Mwang’ondo.
Maofisa wapya wa JWTZ watunukiwa kamisheni Maofisa wapya wa JWTZ watunukiwa kamisheni Reviewed by Zero Degree on 2/04/2018 07:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.