Loading...

Wanachama SADC kufanya uchaguzi mwaka huu

Rais wa DRC, Joseph Kabila
Mataifa matano wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanajiandaa kufanya uchaguzi baadaye mwaka huu wakati huu ambao masuala ya demokrasia na utawala bora yanatupiwa macho katika ukanda huo.

Mataifa hayo ni DR Congo, Madagascar, Msumbiji, Swaziland pamoja na Zimbabwe ambayo uchaguzi wake utakuwa umeunganishwa. Afrika Kusini itafanya mwakani.

Msumbiji imepanga Oktoba 10, 2018 kuwa siku ya uchaguzi katika manispaa zake sita, wakati DRC imetangaza kufanya hivyo Desemba 23 baada ya kucheleweshwa muda mrefu.

Nchi nyingine tatu bado hazijataja tarehe rasmi ya uchaguzi ingawa kwa upande wa Zimbabwe Rais Emmerson Mnangagwa amesema utafanyika Julai.

Uchaguzi wa Zimbabwe utakuwa wa kuchagua rais, wabunge, maseneta na viongozi wa serikali za mtaa.

DRC na Zimbabwe zimehitimisha mchakato wa kuandikia wapigakura, hatua muhimu katika mchakato wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya DRC (CENI) wapigakura 46,021,454 wameandikishwa kupiga kura hadi mchakato wa usajili ulipofungwa Januari 31.

Kati ya walioandikishwa, 24,231,197 ni wanaume na 21,790,257 ni wanawake.

Idadi ya wapigakura waliosajiliwa ni asilimia 48 zaidi ya 31 milioni waliojiandikisha katika uchaguzi uliopita uliofanyika mwaka 2011.

CENI ilisema kampeni za kisiasa zitaruhusiwa mwezi mmoja kabla ya tarehe ya uchaguzi kama ilivyoelekezwa na sheria zinazosimamia uchaguzi nchini DRC.

Katika Zimbabwe, zaidi ya watu 5.3 milioni wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi uliounganishwa. Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) ilisema tayari watu 5,310,734 wameandikishwa kwa mfumo wa BVR zoezi lililodumu kuanzia Januari 10 hadi Februari 8.
Wanachama SADC kufanya uchaguzi mwaka huu Wanachama SADC kufanya uchaguzi mwaka huu Reviewed by Zero Degree on 2/19/2018 01:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.