Loading...

Roy Keane: Anayeikwamisha Manchester United huyu hapa


Roy Keane ana amini klabu ya Manchester United itaendelea kuwa na wakati mgumu katika safu ya ulinzi ikiwa Ashley Young ataendelea kuwa sehemu ya safu hiyo na anakiri kuwa Jose Mourinho inabidi afanye mabadiliko.

Hana imani kwamba Manchester United itaweza kufikia mafanikio inyaoyahitaji kama Young ataendelea kucheza kama beki.

Akizungumza na ITV, Keane alisema kuwa, “Hawajafanya masahihisho ya matatizo waliyokuwanayo katika safu yao ya ulinzi kwa muda mrefu na hilo litaendelea kuwa hivyo.” 

Ashley Young
“Mabeki wawili wa katikati wanatakiwa kufanya vizuri zaidi. Unavyokuwa na Ashley Young katika beki yako, ni dhahiri kuwa utakuwa na wakati mgumu.”

Mashetani wekundu wamepoteza michezo miwili kati ya michezo yao mitatu ya Ligi Kuu ya Uingereza lakini Keane anategemea klabu hiyo itafanikiwa kusonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sevilla.

“Sina shaka na matokeo ya michezo michache ya Ligi Kuu iliyopita,” aliongeza. 

Sevilla itawapa wakati mgumu lakini Manchester United itashinda.

“Watarejea katika hali ya kawaida baada ya michezo kadhaa tu na nafikiri watsonga mbele.”
Roy Keane: Anayeikwamisha Manchester United huyu hapa Roy Keane: Anayeikwamisha Manchester United huyu hapa Reviewed by Zero Degree on 2/16/2018 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.