Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 8 Februari, 2018

Isco
Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa klabu tano zinazopewa nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Isco.

Ripoti zinadai Real Madrid wako tayari kumruhusu Marco Asensio ajiunge na Chelsea kwenye majira ya joto, lakini endapo tu watampata Eden Hazard.

Antonio Conte hajafukuzwa kazi Chelsea kama meneja kwa sababu klabu hiyo ina amini haiwezi kumpata mtu sahihi wa kuchukua nafasi yake. (Express)

Klabu ya Manchester United imepata hasara ya pauni milioni 29 katika kipindi cha miezi mitatu kilichopita.

Craig Bellamy anaamni ni muda mfupi sana umesalia kabla golikipa wa klabu ya Manchester United, David de Gea hajatimkia Real Madrid.

David Unsworth amekataa ofa ya kuwa meneja mpya wa klabu ya Oxford United.

Klabu ya Dundee imethibitisha kumsajili Steven Caulker kama mchezaji huru tangu aondoke QPR. (Sky Sports)

Patrice Evra
Klabu ya West Ham imekamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa Manchester United, Patrice Evra kama mchezaji huru.

Arsenal, Chelsea na Manchestre United wameambiwa wailipie pauni milioni 100 kuipata saini ya Leon Bailey wa Bayer Leverkusen.

Tiemoue Bakayoko: Mimi ni mchezaji bora katika klabu ya Chelsea na Cante ni mdanganyifu. (talkSport)

Uongozi wa Shirikisho la Soka nchini Italia bado haujamkatia tamaa Antonio Conte.

Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Luka Modric amesema kuwa anajutia kuondoka Tottenham katika hali ya kutoelewana.

Winga wa Liverpool, Mohamed Salah amekanusha taarifa zinazomhusisha na Real Madrid.

Meneja wa Chelsea atajilaumu yeye mwenyewe kama atafukuzwa kazi katika klabu ya Chelsea. (ESPN

Luis Enrique
Luis Enrique ni chaguo la kwanza kwa klabu ya Chelsea kuchukua nafasi ya Antonio Conte, lakini kocha huyo wa zamani wa Barcelona hataki kibarua chochote hadi kwenye majira ya joto.

Meneja wa Tottenham, Maurcio Pochettino anasema kuwa Harry Kane pekee ndiye anayeweza kuto jibu juu ya mstakabali wa maisha yake yajayo, huku klabu ya Real Madrid ikionyesha nia ya kutaka kumsajili.

Theo Walcott ana amini Everton itaondokana na kushuka daraja kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, lakini ankiri kuwa kwa sasa matokeo ni muhimu zaidi kuliko utendaji. (Daily Mail)

Kiungo wa Manchester United, Ander Herrera anatuhumiwa kucheza chini ya kiwango kwa makusudi nchini Uhispania.

Liverpool waingia mkataba na mtaalamu wa magolikipa, Hans Leitert kuwasaidia Loris Karius na Simon Mignolet, ingawa Jurgen Klopp anatarajiwa kufanya usajili golikipa mwingine kwenye majira ya joto. (Sun)

Klabu ya Arsenal inafanya mpango wa kumsajili chipukizi wa klabu ya Barcelona, Pablo Moreno kwenye majira ya joto.

Manchester United inakaribia kumnasa beki wa klabu ya Monaco na Timu ya Taifa ya Brazili, Fabinho.

Uwezekano wa klabu ya Manchester City kurejea kuwania saini ya Riyad Mahrez kwenye majira ya joto ni mdogo sana, ikidaiwa kuwa Pep Guardiola hajafurahia tabia za winga huyo tangu dirisha la usajili lifungwe.

Luke Shaw
Luke Shaw anatarajia kupewa mkataba mpya katika klabu ya Manchester United kabla ya kuisha kwa msimu huu.

Kiungo wa Shakhtar Donetsk, Fred atajiunga na Manchester City, kwa mujibu wa Mircea Lucescu, ambaye ndiye alimsajili nyota huyo katika klabu hiyo ya Ukrain. (Mirror)

Luis Enrique anataka kazi yake ijayo ya ukufunzi iwe ni katika Ligi Kuu ya Uingereza na anajiandaa kwenda nchini Uingereza.

Meneja mpya wa Stoke City, Paul Lambert anasema kuwa hajali kama hakuwa chaguo la kwanza la klabu hiyo kuchukua nafasi ya Mark Hughes kwani alikuwa amekumbuka sana kazi hiyo kwenye Ligi Kuu ya Uingerezaa. (Telegraph)

Jack Hendry anasema kuwa alikataa ofa za kutoka vilabu kadhaa vya Uingereza na kuchagua kujiunga na klabu ya Celtic.

Shirikisho la Soka la Uskoti (SFA) linasema kuwa linaweza kuteua meneja mpya wa Timu ya Taifa ya Uskoti kabalya kuteua Mkurugenzi Mkuu ili kutafuta mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya Stewart Regan. (Record)

Real Madrid ilipewa ofa ya kumsajili Alexis Sanchez na klabu ya Arsenal lakini meneja wa klabu hiyo, Zinedine Zidane alikataa.

Riyad Mahrez ameonywa ya kwamba hatalipwa mshahara wake kama hatarejea Leicester. (Star)

Marco Silva anaitishia kuichukulia klabu ya Watford hatua za kisheria kama hatalipwa fedha zake za fidia.
 (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 8 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 8 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/08/2018 06:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.