Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 4 Februari, 2018

Neymar Jr
Barcelona inadai Neymar ndiye aliyesababisha ongezeko kubwa katika ada za uhamisho wa wachezaji. (ESPN)

Klabu ya Liverpool inahofia ushindani kutoka Real Madrid kwenye mbio za kuwania saini nyota wa Roma, Allison Becker.

Meneja wa Southampton, Maurcio Pellegrino ana matumaini kuwa ushindi wa klabu hiyo dhidi ya West Brom utaowangezea wachezaji wake kujiamini.

Klabu ya Everton imempa ruhusa David Unsworth kuzungumza na Oxford United juu ya nafasi ya kazi ya umeneja.

Aliyekuwa meneja wa Swansea, Paul Clement ana uhakika kiwango cha Renato Sanchez kitaimarika ndani ya muda mfupi katika dimba la Liberty.

Oliver Giroud amesema kuwa klabu nyingi kubwa za Ulaya zilikuwa zinaitaka saini yake. (Sky Sports)

Kwa mujibu wa aliyekuwa kiungo wa Liverpool, Graeme Souness, mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane yupo tayari kujiunga na klabu ya Real Madrid lakini muda wa Dele Alli bado haujafika. (Times )

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp anatarajia Manchester City itakuwa na nguvu zaidi msimu ujao kuliko sasa.

Hugo Lloris
Hugo Lloris amewataka wachezaji wenzake wa Tottenham wacheze kwa umoja kuishusha Liverpool kutoka nafasi ya tatu. (Observer)

Antonio Conte anaweza kufukuzwa kazi endapo klabu ya Chelsea itapoteza mchezo wake dhidi ya Watford siku ya Jumatatu. (Express)

Manchester United inafanya mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya Bayern Munich, Arturo Vidal.

Tottenham inaweza kuwa tishio kwa Manchester City, kwa mujibu wa Glenn Hoddle.

Mashabiki wa Everton waliondoka uwanjani baada ya kipindi cha kwanza kuisha, klabu yao ikiwa imefungwa goli 4-0. (Daily Mail)

Manchester United iko kwenye mazungumzo na klabu ya Ajax juu ya uhamisho wa wingwa wa klabu hiyo ya Uholanzi, Justin Kluivert kwenye majira ya joto.

Jurgen Klopp amedai kwamba Ligi Kuu ya Uingereza ni ngumu sana hata aliyekuwa meneja wa zamani wa klabu ya Liverpool, Bill Shankly atafurahia endapo klabu hiyo itamaliza katika nafasi ya nne.

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp anasisitiza kuwa mshambuliaji wa klabu hiyo, Sadio Mane hana wivu na mchezaji mwenzake, Mohamed Salah na kusema kwamba wawili hao ni 'marafiki wa dhati'.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amemzuia msaidizi wake, Mikel Arteta kujiunga na timu ya taifa ya Wales. (Mirror)

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anasisitiza kwamba anataka wachezaji wiwili au watatu wenye uwezo mkubwa awez kushindana na klabu ya Manchester City.

Meneja wa Newcastle, Rafa Benitez anataka kufuata nyayo za Roy Hodgson na afanye kazi ya umeneja akiwa miaka ya 70.

Ross Barkley
Ross Barkley anatarajiwa kuikosa mechi ya Chelsea dhidi ya Watford baada ya kupata majeraha ambayo yanaweza kumweka nje kwa muda usiojulikana chini ya meneja wake, Antonio Conte. (Telegraph)

Arsenal na Chelsea zimejiunga na Manchester City kwenye vita ya kuwania saini ya Riyad Mahrez kwenye majira ya joto.

Manchester City inashughulikia mkataba mpya wa Gabriel Jesus. (Star)

Conte anaweza kufukuzwa kazi Chelsea siku ya Jumatatu na klabu hiyo iko tayari kulipia pauni milioni 7 kumnasa atakayechukua nafasi yake.

Liverpool inahitaji kiungo mwingine kutoka Emirates baada ya kumnasa Alex Oxaled-Chamberlain. (talkSport)

Manchester United ataelekeza nguvu zake kwa Jordan Pickford kama David De Gea ataondoka mwishoni mwa msimu.

Chelsea ina wakati mgumu kumbakisha Thibaut Courtois - na inataka kumsajili Joe Hart achukue nafasi yake.

Jack Wilshere
Liverpool inamtaka Jack Wilshere - kama nyota huyo atakataa kusaini mkataba mpya katika klabu ya Arsenal.

Riyad Mahrez amepewa msaada na PFA kwenye mgogoro wake na klabu ya Leicester.

Arsenal inataka pauni milioni 15 ili amwachie Rob Holding, beki huyo akielekea kuondoka katika klabu yake mwishoni mwa msimu.

Celtic na Rangers zitagombania saini ya chipukizi wa klabu ya Sunderland, Ethan Robson kwenye majira ya joto. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 4 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 4 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/04/2018 06:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.