Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 7 Februari, 2018

Lionel Messi
Lionel Messi alikataa ofa ya mataba wa pauni milioni 88 kwa mwaka kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya China na kuchagua kubaki Barcelona.

Ryan Giggs anaamini Jose Mourinho bado ana nafasi ya kutwa taji la Ligi Kuu ya Uingerza kama atafanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake.

Nyota wa klabu ya Liverpool, Emre Can ameshakubali kujiunga na Juventus, kwa mujibu wa wakala wake.

Mafanikio ya Gareth Bale katika klabu ya Real Madrid yanaweza kumsahwishi Harry Kane aondoke Tottenham.

Golikipa wa klabu ya Chelsea, Thibaut Courtois amesema kuwa 'moyo wake uko Real Madrid'. (Mirror)

Antonio Conte ataondoka katika klabu ya Chelsea kwenye majira ya joto, kwa mujibu wa Ian Wright.
Aubameyang na Mkhitaryan
Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerikh Aubameyang anasema kuwa uhamisho wa Henrikh Mkhitaryan kwenda Arsenal ulichangia kwa kiasi kikubwa kumfanya aamue kujiunga na klabu hiyo. (Sky Sports)

Patrice Evra atajiunga na klabu ya West Ham kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Marseille kuvunjwa.

Antonio Conte anabakia kuwa meneja wa Chelsea, huku wachezaji wake wakiwa kwenye mapumziko ya siku 3.

Thibaut Courtois atafanya mazungumzo na klabu ya Chelsea juu ya mkataba mpya licha ya kuhusishwa na kujiunga na Real Madrid.

Klabu ya Leicester City 'imejiandaa kumvumilia' Riyad Mahrez pamoja na mgomo wake.

Nyota wa klabu ya Manchester United, Alexis Sanchez amehukumiwa kwenda jela kwa miezi 16 kisa kodi ambazo hazijalipwa - lakini nyota huyo anaweza kuepuka adhabu hiyo kwa kulipa kiasi cha pauni 890,000. (talkSport)

Kibarua cha Antonio Conte kama meneja wa klabu ya Chelsea kiko salama licha ya kudhdririshwa na Watford kwa kichapo cha goli 4-1.

Meneja wa Tottenham, Maurcio Pochettino amemkingia kifua Alli kwa kusema kuwa kitendo cha kumdanga mwamuzi na adui wako katika mechi ni sehemu ya mchezo.

Marco Reus
Borussia Dortmund imetoa ofa ya mkataba mpya kwa kiungo wa klabu hiyo na timu ya taifa ya ujerumani, Marco Reus. (ESPN)

Manchester United inahitaji kiasi cha pauni milioni 115 kumwachia David de Gea na Real Madrid inatarajiwa kuanza upya mchakato wa kumnasa golikipa huyo.

Kitendo cha Thomas Lemar kugoma kusaini mkataba mpya katika klabu ya Monaco kimezichochea Arsenal na Liverpool kuendeleza harakati za kuiwania saini ya Mfaransa huyo.

Baada ya kumnasa Sagna, klabu ya Benevento sasa iko inafukuzia saini ya nyota wawili wa zamani wa Arsenal, Samir Nasri na Alexander Song.  

Msako wa golikipa unaofanywa na klabu ya Real Madrid unatarajiwa kuisha kwa kumsajili Courtois, huku Mbelgiji huyo akionekana kuwa na matamnio makubwa ya kujiunga na vigogo hao wa La Liga. 

Luis Enrique amekubali dili la kujiunga na klabu ya Chelsea kuchukua nafasi ya Antonio Conte na anategemewa kusaini mkataba utakaomweka Stamford Bridge hadi 2020. (Daily Mail)

Riyad Mahrez ataikosa mechi dhidi ya Manchester City wikendi ijayo, huku mgomo wake katika klabu hiyo ukiendelea.

Enrique atamsajili Luis Suarez kama atafanikiwa kuchukua nafasi ya Antonio Conte kama meneja wa Chelsea mwisho wa msimu huu.

Arsenal ina mpango wa kumsajili beki wa klabu ya Juventus, Daniele Rugani.

Klabu ya Chelsea itamfukuza kazi Antonio Conte kama atashindwa kumaliza ligi katika nafasi nne bora.

Naby Keita
Meneja wa RB Leipzig amesema kuwa dili la uhamisho wa Naby Keita kwenda Liverpool limeathiri kiwango cha nyota huyo. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 7 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 7 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/07/2018 01:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.