Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 19 Februari, 2018

Kylian Mbappe
Kylian Mbappe atakamilisha rasmi uhamisho wake kwenda PSG kutoka Monaco moja kwa moja kwa kiasi cha pauni milioni 166.

Baba mzazi wa James Rodriguez anadai kuwa mwanaye alifanya jambo jema sana kuamua kuondoka Real Madrid na kwenda Bayern Munich kwa uhamisho wa mkopo.

Mechi ya wapinzani wa jadi nchini Brazil, kati ya Vitoria na Bahia iliahirishwa baada ya wachezaji tisa kutolewa nje kwa sababu ya vurugu. (Daily Mail)

Eden Hazard amezima uvumi unaomhusisha na uhamisho kwenda Real Madrid kwa kusisitiza kuwa anafurahia kuitumikia klabu ya Chelsea.

Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardioala amsema kuwa alikaribia kujiunga na klabu ya Wigan kama mchezaji siku za nyuma. (Sky Sports)

Klabu ya Tottenham inajiandaa kutumia pauni milioni 50 kuwanasa nyota wawili wa klabu ya Watford, Richarlison na Abdoulaye Doucoure.

Klabu ya Chelsea haina uwezo tena wa kushindana na Manchester United na Manchester City kwenye suala zima la usajili wa wachezaji wenye uwezo mkubwa, kwa mujibu wa Graeme Souness. (talkSport)

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amemfanya kiungo wa Schalke 04, Max Meyer kuwa chaguo lake la kwanza kwenye usajili wa majira ya joto.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amemwambia Claudio Bravo kuwa bado yuko kwenye mipango ya kikosi cha klabu hiyo. (Star)

Marcos Rojo
Jose Mourinho anachukizwa na kitendo cha mazunguzo ya mkataba mpya wa Marcos Rojo kucheleweshwa - huku klabu ya PSG ikiwa tayari kumnasa nyota huyo wa Manchester United.

Real Madrid wanataka kumuuza Gareth Bale kwa zaidi ya pauni milioni 100 ili kumununua mashambuliji wa klabu ya Chelesea, Eden Hazard.

Mmiliki wa klabu ya West Brom, Guochan Lai ametoa mechi mbili kwa meneja wa klabu hiyo, Alan Pardew kuinusuru kazi yake kwa sababu za kinidhamu na  matokeo mabovu ya timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

AC Milan na Inter Milan zitashindania saini ya mshambuliaji kutoka Nice, Mario Balotelli.

Manchester United naHuddersfield zinasubiria uamuzi wa FA baada ya mashabiki kuvamia uwanjini baada ya goli la Romelu Lukaku siku ya Jumamosi. (Sun)

Carlo Ancelotti hana nia ya kurejea katika klabu ya Paris Saint-Germain kwa sababu matazamio yake kwa sasa ni kurudi Ligi Kuu ya Uingereza.

Lengo kuu la kiungo wa klabu ya Watford, Abdoulaye Doucoure ni kuja kuichezea timu yake ya Taifa ya Ufaransa.

Winga wa klabu ya Benifica, Andre Carrillo anayeichezea Watford kwa mkopo, atajiunga na klabu hiyo ya Uingereza moja kwa moja kwenye majira ya joto.

Michy Batshuayi
Klabu ya Chelsea ilikataa kumruhusu Michy Batshuayi ajiunge na Borussia Dortmund kwa mkataba wa kudumu kwa sababu bado inafikiria kuwa nyota huyo atang'ara Stamford Bridge kwa baadae. (Mirror)

Klabu ya Chelsea haiko tayari kumwachia Eden Hazard labda kama itampata Sergio Aguero kama sehemu ya makubaliano yao.

Marco Reus amefunga goli lake la kwanza tangu kurejea kwake katika klabu ya Borussia Dortmund akitokea majeruhi.

Klabu ya Manchester United ina matumaini kiungo wa klabu hiyo, Paul Pogba atakuwa fiti kuivaa Sevilla. (ESPN)

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba anaweza kurejea moja kwa moja ndani ya kikosi cha kwanza cha Manchester United kitakachocheza dhidi ya Sevilla kwenye Klabu Bingwa.

Jonny Evans
Nahodha wa klabu ya West Brom, Jonny Evans atapewa kial nafasi ajikomboe baada ya mkufunzi mkuu, Alan Pardew kumvua kitambaa cha unahodha katika mechi ya michuano ya FA dhidi ya Southampton Jumamosi. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 19 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 19 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/19/2018 08:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.