Loading...

TFF yamfungia Juma Nyoso

Juma Nyoso
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) kupitia Kamati yake ya Nidhamu imemshushia adhabu kali mchezaji wa Kagera Sugar, Juma Nyoso kwa kosa la kumpiga shabiki baada ya mechi kati ya timu yake na Simba SC.

Kamati hiyo ya TFF iliyokutana Jumamosi iliyopita Februari 10, 2018 imemfungia Nyoso mechi tano na kumpiga faini ya shilingi 1,000,000 (Milioni moja) baada ya kikao hicho kujiridhisha kuwa mchezaji huyo alimpiga shabiki huyo.

Nyoso alimpiga shabiki baada ya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya timu yake ya Kagera Sugar dhidi ya Klabu ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
TFF yamfungia Juma Nyoso TFF yamfungia Juma Nyoso Reviewed by Zero Degree on 2/13/2018 07:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.