Eden Hazard ataja wachezaji bora watatu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza
Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea na Timu ya Taifa ya Ubelgiji, Eden Hazard |
Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, nyota huyo wa Chelsea alisema: “Nafikiri kuna wachezaji bora watatu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza – Kevin De Bruyne, Mohamed Salah and Harry Kane.”
Hazard aliendelea kwa kusema kuwa kura yake ya mchezaji bora wa PFA alimpigia Mbelgiji mwenzake anayekipiga Manchester City. “Nilimpigia kura Kevin De Bruyne. Yeye ni mchezaji bora zaidi. Ningeweza kumpigia kura Salah kwa sababu nimecheza naye na ni rafiki yangu laiki Salah ni mshambuliaji zaidi kuliko mchezaji.
“Kevin ana kila kitu. Anaweza kuzui (kucheza kama beki), kutoa pasi, assist (pasi ya mwisho) na kufunga magoli kwenye mechi kubwa. Kwangu mimi, yeye ndio bora zaidi kwa msimu huu.”
Kevin de Bruyne, Mo Salah na Harry Kane ndio wachezaji waliong'ara zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu |
Huku vijana wa Pep Guardiola wakikaribia kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza, De Bruyne ana nafasi kubwa ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka. Lakini Salah na Kane wanaweza kuleta ushindani mkubwa.
Eden Hazard ataja wachezaji bora watatu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza
Reviewed by Zero Degree
on
3/05/2018 03:40:00 PM
Rating: