Loading...

Makamu wa rais TFF kuhojiwa na Kamati ya Maadili


Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imempeleka Makamu wa Rais wa shirikisho hilo, Michael Wambura katika Kamati ya Maadili na Sekretarieti yake, kwa tuhuma za uvunjifu wa kanuni za maadili.

Kamati hiyo imekutana leo Machi 14, 2018 kujadili tuhuma zinazomkabili Wambura ikiwemo ya kupokea na kuchukua fedha za TFF za malipo ambayo hayakuwa halali, kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali.

Tuhuma nyingine ni kufanya vitendo vinavyoshusha hadi ya TFF kinyume na sheria na katiba ya shirikisho hilo.

Shauri hilo la Wambura limefikishwa kwenye kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali, ambapo suala hilo la Wambura lilionekana linatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili.

Kamati ya Maadili imepokea malalamiko yanayomuhusu Wambura ikiwa ni uvunjifu wa kanuni za Maadili Tolea la 2013 na Katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa mwaka 2015.

Wito huo umemtaka Wambura kufika mbele ya Kamati ya Maadili baadaye leo na ana hiyari ya kufika kutoa utetezi huo kwa njia ya mdomo,kutuma kwa maandishi,kuleta mashahidi au kutuma muwakilishi akiambatana na barua ya uwakilishi.
Makamu wa rais TFF kuhojiwa na Kamati ya Maadili Makamu wa rais TFF kuhojiwa na Kamati ya Maadili Reviewed by Zero Degree on 3/14/2018 08:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.