Loading...

Real Madrid yaikatisha tamaa Liverpool kwa Mbrazil huyu


Real Madrid imemfanya golikipa wa klabu ya Roma, Alisson Becker kuwa chaguo lao la kwanza, kwa mujibu wa ripoti zilizotoka nchini Uhispania.

Madrid imekuwa kwenye msako kwa muda mrefu kutafuta golikipa mwenye viwango vya kimataifa na baada kuahirisha kumsajili golikipa wa Athletic Club, Kepa Arrizabalaga mwezi Januari, mabingwa hao wa UEFA wamekuwa wakihusishwa na magolikipa wa Manchester United, David De Gea na Chelsea, Thibaut Courtois.

Sasa wamegeukia kwa Alisson, na wamemfanya golikipa huyo kutoka Brazil kuwa chaguo lao la kwanza kwenye majira ya joto. Huku De Gea na Courtois wakithibitisha kwamba watabaki Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao.

Alison Becker
Alisson amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Ligi Kuu ya Uingereza hivi karibuni, huku Liverpool ikiripotiwa kuwa na hamu ya kumnasa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25.

Hata hivyo, matumaini ya klabu ya Liverpool kumshawishi Alison atue Anifield yamepotea baada ya Real Madrid kuingia kwenye mbio za kuwania saini ya Mbrazil huyo.

Golikipa huyo amechezea Roma kila mchezo wa Ligi Kuu na michuano ya Ulaya hadi hivi sasa msimu huu, akifanikiwa kucheza michezo 17 bila kufungwa.

Pia amecheza mechi 14 bila kufungwa kati ya mechi 23 akiwa na timu ya taifa ya Brazil.
Real Madrid yaikatisha tamaa Liverpool kwa Mbrazil huyu Real Madrid yaikatisha tamaa Liverpool kwa Mbrazil huyu Reviewed by Zero Degree on 3/28/2018 12:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.