Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Machi, 2018

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger
Bodi ya ya Arsenal pamoja na wachezaji wa klabu hiyo wameanza kumgeuka Arsene Wenger, huku kukiwa na orodha ya makocha waliondaliwa kuwania nafasi yake.

Nahodha wa klabu ya Liverpool, Jordan Henderson anasema kuwa ana amini klabu hiyo ni moja kati ya klabu bora zaidi duniani.

Alan Pardew anatarajiwa kubadilisha mfumo wake ili kujaribu kuokoa kibarua chake katika klabu ya West Brom.

West Ham itangia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya beki wa klabu ya West Brom, Jonny Evans mwihsoni mwa msimu huu, huku Leicester na Everton pia zikiwa na matamanio makubwa ya kumnasa nyota huyo. (Mirror)

Jack Wilshere yuko tayari kuondoka katika dimba la Emirates kama mchezaji huru kwenye majira ya joto, isipokuwa kama klabu ya Arsenal itaboresha maslahi ya mkataba wake wa sasa.

Manchester City imemwambia Raheem Sterling kuwa atalazimika kusubiri hadi mwisho wa msimu ndio atapa nafasi ya kufanya mazungumzo juu ya mkataba mpya.

Jan Oblak amesaini mkataba mpya na klabu ya Atletico Madrid, na kuzikatisja tamaa Chelsea, Arsenal, Liverpool na PSG, ambazo zilikuwa zinawania saini ya golikipa huyo.

Mwenyekiti wa klaby ta Crystal Palace, Steve Parish amesema kuwa klabu hiyo tayari ilishaanza kufanya mipango ya michuano ya Ligi daraja la kwanza kama ikitokea ikashuka daraja msimu huu.

Meneja wa kalbu ya Birmingham, Steve Cotterill amepewa muda wa uchunguzi na mmiliki wa klabu hiyo. (Sun)

Steven Piennar
Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Everton, Tottenham na Timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Steven Piennar ametangaza kustaafu kucheza soka. 

Mshambuliaji wa PSG, Neymar JR atafanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki hii nchini Brazil.

Klabu ya Beskitas imemsajili Jermain Lens kwa mkataba wa moja kwa moja kutoka Sunderland.

Etienne Capoue amesaini mkataba mpya katika klabu ya Watford utakaoisha mwaka 2022.
 
Manchester United imeongeza mikataba ya Asley Young na Daley Blind hadi mwaka 2019. (Sky Sports)

Kamishina msaidizi wa Shirikisho la Soka la Italia, Alessandro Costacurta amethibitisha kuwa Antonio Conte ndiye chaguo lao la kwanza.

Manchester United ina mpango wa kumsajili Willian kutoka Chelsea kwa pauni milioni 40 kwenye majira ya joto.

Kiungo wa klabu ya Atletico Madrid, Thomas Partey amesaini mkataba mpya utakaoisha mwaka 2023.
 
Frank Lampard ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuchukuwa nafasi ya Antonio Conte katika klabu ya Chelsea. (ESPN)

Declan Rice
West Ham inataka kutoa ofa ya mshahara wa pauni 25,000 kwa wiki kwa beki wake chipukizi, Declan Rice. 

Klabu ya Manchester United inatarajiwa kuahirisha mipango yake ya kuufanyia maborehso uwanja wa Old Trafford na badala yake itampa fedha meneja wake, Jose Mourinho kwa ajili ya usajili wa wachezaji kwenye majira ya joto.

Chelsea itachelewesha mazungumzo juu ya mkataba mpya na Thibaut Courtois hadi baada ya michezo yao dhidi ya Leicester na Barcelona, huku kukiwa na tetesi zinazomhusisha na uhamisho kwenda Real Madrid. (Daily Mail)

Nyota wa klabu ya Roma, Allesandro Florenzi, ambaye anawaniwa na Chelsea pamoja na Manchester United anasita kusaini mkataba mpya katika klabu yake.

Arsene Wenger ana imani Jack Wilshere atakubali kusaini mkataba mpya katika klabu ya Arsenal. (talkSport)

Golikipa wa Burnley, Nick Pope
Gareth Southgate atamchunguza golikipa wa klabu ya Burnley, Nick Pope kwa mara ya pili, huku akiendelea kufikiria kumuita kinda huyoo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki Kombe la Dunia. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 1 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/01/2018 11:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.