Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 15 Machi, 2018
Andres Iniesta |
Nahodha wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta anasema kuwa anatafakari juu ya uhamisho wake kwenda China kwenye majira ya joto.
Kevin De Bruyne ana hamu ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Manchester United.
Ryan Sessegnon ameitwa kwa mara kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.
Aaron Ramsey ameachwa nje ya kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Wales chini ya mkufunzi mpya, Ryan Giggs.
Meneja wa Barcelona, Ernesto Valverde amesena kuwa hana uhakika kama Andres Iniesta ataendelea kuwepo katika klabu hiyo.
Kocha mkuu wa klabu ya Hirbenia, Neil Lennon amefungiwa mechi tano kufuatia vitendo vyake vya utovu wa nidhamu. (Sky Sports)
Manchester City wanakaribia kusaini mkataba wenye thamani ya pauni milioni 45 kwa mwaka na Kampuni ya Puma kama mdhamini wao mpya.
Hatimaye, Chelsea wako huru kuendelea na maboresho wa uwanja wao kwa pauni bilioni 1 baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano na familia iliyokuwa inazuia mpango huo.
Patrick Kluivert amepujipunguzi nafasi ya uwezekano wa kuwa meneja wa klabu ya Oxford United baada ya kukataa kuhudhuria mkutano.
Everton wanamnyatia beki wa Basel, Leo Lacroix anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 7.5 ili kuiongezea nguvu safu yao ya ulinzi. (Sun)
Maxime Gonalons |
Klabu ya Villareal inamnyatia kiungo wa klabu ya Roma na timu ya taifa ya ufaransa, Maxime Gonalons.
Real Madrid wanaamini kwamba, dau la pauni milioni 300 linaweza kuishawishi PSG ikubali kumuuza Neymar kwenye majira ya joto. (Marca)
Urusi yatishia kuzuia vyombo vya habari vya Uingereza kuhudhuria kombe la Dunia.
Vigogo ndani ya Old Trafford wanahoji kama Jose Mourinho ni mtu sahihi wa kuiongoza Manchester United baada ya timu yao kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa. (Daily Mail)
Liverpool itatoana jasho na Tottenham kumsajili beki wa klabu ya Stuttgart, Benjamin Pavard anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30.
Bayern Munich iko tayari kujiunga na Juventus kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo kutoka Liverpool, Emre Can. (Mirror)
Cologne iko hatarini kumpoteza beki wake, Jonas Hector kama itashuka daraja msimu huu.
Mitchell Weiser ndio chaguo la kwanza kwa Bayer Leverkusen, ingawa vilabu vingi kutoka Uingereza, Italia na Ujerumani vinawania saini ya beki huyo wa klabu ya Hertha Berlin. (Kicker)
Mshambuliaji Saido Berahino anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Stoke City wikendi hii. (Telegraph)
Luka Modric |
Arsenal wako tayari kutumia pesa nyingi kumrejesha Luka Modric kwenye Ligi Kuu ya Uingereza wakati wa majira ya joto lakini wanakabiliana na ushindani mkubwa kutoka Liverpool na Spurs.
Arsene Wenger amechagua kutofuatilia usajili wa nyota wa Chelsea, Willian - iwa na skauti wake. (Express)
Nyota wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata anaweza kuingia matatani baada ya kitendo alichowafanyia mashabiki wa Barcelona. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 15 Machi, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
3/15/2018 11:24:00 AM
Rating: