Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 22 Machi, 2018

Alexis Sanchez
Alexis Sanchez amekiri kuwa na hali ngumu sana tangu ajiunge na Manchester United akitokea Arsenal.

Arsenal imemwambia Jack Wilshere kuwa yuko huru kuondoka kama atapata mkataba kutoka klabu nyingine.

Mashabiki watano wa klabu ya West Ham wamefungiwa kutazama soka maisha yao yote kwa kuvamia uwanjani. (talkSport)

Diego Costa ana amini kuwa ingekuwa jambo jema kama Antoine Griezmann atabaki Atletico Madrid kwa msimu mwingine zaidi.

Ashley Williams anakiri kuwa alifikiria kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Wales baada kushindwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia.

Jack Wilshere amekiri kwamba, angependelea suala la mkataba wake katika klabu ya Arsenal lishighulikiwe kabla ya Kombe la Dunia.

Usain Bolt atafanya mazoezi pamoja na klabu ya Borussia Dortmund siku ya Ijumaa. (Sky Sports)

Jordan Pickford anatarajiwa kuanza na kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya Uholanzi Ijumaa. (Guardian)

Mkurugenzi wa kandana wa klabu ya Bayern Munich, Hasan Salihamidzic ameulizea uwezekano wa kumsajili nyota wa Cologne, Jonas Hector. 

Bayern Munich hatimzuia Juan Bernat kama atataka kuondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto. (Kicker)

Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Barcelona, Ronaldinho Gauchi anatarajiwa kuwania ubunge katika taifa lake la Brazil.

Wachezaji wa Uingereza wamepewa vipimo vyenye utata kupima ugonjwa wa pumu kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia.

Paulo Dybala
Atletico Madrid italazimika kulipa pauni milioni 105 kama itataka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Juventus, Paulo Dybala kwenye majira ya joto.

Liverpool wanatarajiwa kupanua uwanja wa Anfield kwa mara nyingine tena, klabu hiyo ikiwa na lengo la kuwa na viti 60,000 na mdhamini mkubwa kubeba jina la uwanja mpya. (Daily Mail)

Liverpool ina uhakika wa kuzipiku Manchester United na Arsenal kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho kwenye majira ya joto, wakati Emre Can akielekea kuondoka Anfield.

Meneja wa Burnley, Sean Dyche atatoa ofa ya pauni milioni 10 kwa ajili ya beki wa West Brom, Craig Dawson kwenye majira ya joto.

Manchester United ina mpango wa kumsajili beki wa klabu ya Real Madrid, Raphael Varane kwa pauni milioni 50 kwenye majira ya joto.

Yaya Toure ameshindwa kurejea dimbani akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa ya Ivory Coast kwa sababu za kifamilia. 

Burnley itajiunga na mbio kuwania saini ya beki wa klabu ya West Brom, Craig Dawson kwa dau la pauni milioni 10 kama itashuka daraja. (Mirror)

Dele Alli  na mkufunzi wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate
Dele Alli ana amini kwamba, kitendo cha kupoteza mchezo wao dhidi ya Iceland kwenye michuano ya Euro mwaka 2016 kimeifanya Uingereza kuwa na nguvu kuelekea Kombe la Dunia nchini Urusi.

Erik Pieters amepigwa faini ya pauni 70,000 na Stoke City kwa kukiuka kanuni na taratibu za klabu siku moja kabla ya mchezo wao dhidi ya Everton.

Ross Barkley anatarajiwa kurejea katika mazoezi ya Chelsea wiki ijayo kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Antonio Conte kwa wiki kadhaa zilizosalia kabla msimu haujaisha. (Telegraph)

Meneja wa Southampton, Mark Hughes anataka kumsajili nyota wa klabu ya Stoke City, Xherdan Shaqiri kwa pauni milioni 20 kwenye majira ya joto.

Manchester United wanafanya mpango wa kumrejesha Cristiano Ronaldo katika dimba la Old Trafford, Alexis Sanchez akitarajiwa kuondoka. (Express)

Chelsea na Real Madrid zitashindania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan, Mauro Icardi kwenye majira ya joto.

David Luiz
David Luiz anatazamia kuisaidia klabu yake kumaliza ligi katika nafasi ya nne baada ya kurejea kikosini akitokea Uhispania kwa matibabu ya goti. (Sun)

Brendan Rodgers anasisitiza kuwa Celtic iko tayari kwa dau litakalotajwa na PSG kwa ajili ya usajili wa Odsonne Edouard moja kwa moja. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 22 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 22 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/22/2018 01:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.