Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 23 Machi, 2018
Real Madrid imekubali ofa ya pauni milioni 130 kwa ajili ya Gareth Bale kutoka klabu ya Ligi kuu ya China. (talkSport)
Gerard Pique ana amini kuwa Pep Guardiola alipoteza imani naye kabla kocha huyo hajaacha kuinoa Barcelona mwaka 2012.
Klabu ya AFC Wimbledon imemsajili aliyekuwa winga wa Charlon, Llyoyd Sam kwa mkataba wa muda mfupi.
Timu ya Taifa ya wanawake ya Uingereza imepanda hadi nafasi ya pili Duniani katika viwango vipya vya FIFA.
Oliver Giroud anakiri kuwa alitegemea kufunga magoli mengi akiwa na Chelsea.
Klabu ya Reading imethibitisha kumteua aliyekuwa mkufunzi wa Swansea, Paul Clement kuwa meneja wao mpya. (Sky Sports)
Gareth Bale anasema kuwa anajisikia vizuri kuwa kuongoza kwa kufumania nyavu Wales kuliko kushinda Taji la Ligi ya Mabingwa akiwa na Real Madrid.
Alexis Sanchez |
Alexis Sanchez amekiri kwamba ''amechoka kisaikolojia na kihisia'', huku akiwa na hali ngumu kuweza kuendana na mfumo wa Manchester United.
Meneja wa Uholanzi, Ronald Koeman amekiri kwamba alistahili kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya David Platt wa Uingereza mwaka 1993.
Argentina inaweza kuwa na mgogoro na klabu ya Manchester City juu ya hali ya Sergio Aguero.
Usain Bolt ameumgana na Borussia Dortmund kwa siku yake ya kwanza ya mazoezi.
Aliyekuwa nyota wa klabu ya Arsenal, Alexander Hleb amesema kuwa atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu baada ya kujiunga na BATE Borisov kwa mara yake ya tano.
Babu yake na Lewis Cook anatarajia kuingiza pauni 17,000 kama kiungo huyo wa Bournemouth atacheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Uingereza katika mechi zijazo dhidi ya Uholanzi au Italia. (Sun)
Klabu ya Tottenham inatazamia kumsajili bekiwa West Brom, Jonny Evans achukue nafasi ya Toby Alderweireld.
Ryan Sessegnon |
Beki wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon ameambia asiwe na wasiwasi juu ya nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye majira ya joto.
Jurgen Klopp amesema aliutazama mara nne mchezo wake wa kwanza kama meneja ndani ya usiku mmoja. (Mirror)
Beki wa klabu ya St Pauli, Lasse Sobiech atajiunga na Cologne mwishoni mwa msimu huu, wakati mkataba wake utakapoisha. (Kicker)
Klabu ya Rangers imemrejesha Louis Moult kwenye rada zake -huku straika huyo wa zamani wa Motherwell akiwa na wakati mgumu Preston. (Daily Mail)
Jose Mourinho anakabiliwa na wakati mgumu kuwaimarisha Alexis Sanchez na Paul Pogba, huku ikidaiwa kuwa wawili hao hawo katika hali ya kimchezo Man United. (Telegraph)
Kiungo wa Real Madrid, Toni Kross amesema kuwa anatamani Neymar ajiunge naye katika dimba la Santiago Bernabeu msimu ujao.
Kiungo wa klabu ya Eintracht Frankfurt Omar Mascarell amekiri kuwa angependa kurejea Real Madrid. (AS)
Gareth Southgate anatarajia kuachana na Harry Kane kwa kumfanya Jordan Henderson kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia.
Beki wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, Seamus Coleman alikuwa na imani kwamba siku moja atarejea kwenye kiwango chake cha juu baada ya kuvunjika mguu. (Express)
Mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud amesema kuwa anaumizwa na suala la kukosa magoli ya kutosha msimu huu. (Star)
Rafael Leao |
Mshambuliaji wa Sporting Lisbon, Rafael Leao, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Tottenham na Manchester City hatauzwa kwenye majira ya joto.
Tom Rogic bado hajatoa uamuzi wake juu ya mstakabali wa maisha yake yajayo katika klabu ya Celtic. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 23 Machi, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
3/23/2018 10:29:00 AM
Rating: