Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 30 Machi, 2018
Robert Lewandowski |
Mkufunzi wa klabu ya Bayern Munich, Jupp Heyncakes anaamini kuwa Robert Lewandowski ataachana na uhamisho kwenda Real Madrid kusalia na vigogo hao wa Ujerumani kwa lengo la kuivunja rekodi yake.
Kwa mujibu wa Sebastian Veron, Jose Muorinho inabidi ampe uhuru Alexis Sanchez na mashabiki wa timu hiyo inabidi wawe wavumilivu.
Antonio Conte anasema kuwa Tottenham ina uwezo wa kumudu mchezo bila Harry Kane. (ESPN)
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa klabu yake haina mpango wa kumuuza Isco kwenye majira ya joto.
Jose Mourinho amekana kufanya mazungumzo na mkufunzi wa timu ya taifa ya Ufaransa juu ya namna ya kumtumia Paul Pogba uwanjani.
Kiungo wa Shakhtar Donetsk, Fred anapendelea kujiunga na Ligi Kuu ya Uingereza, kwa mujibu wa mshauri wake na aliyekuwa nyota wa Arsenal, Gilberto.
Zinedine Zidane amesema kuwa anataka kubakia kama mkufunzi wa klabu ya Real Madrid.
Meneja wa Aston Villa, Steve Bruce amesema kuwa angependelea kama John Terry angaesalia katika klabu hiyo msimu ujao. (Sky Sports)
Manchester United wako tayari kuutumia mgogoro wa makataba mpya kati ya Samuel Umtiti na klabu ya Barcelona.
Fyodor Smolov |
West Ham wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa nahodaha wa Urusi, Fyodor Smolov kwenye majira ya joto.
Meneja wa klabu ya Lincoln, Danny Cowley anapewa nafasi kubwa ya kumrithi Mick McMarthy katika klabu ya Ipswich mwishoni mwa msimu huu.
QPR itawauza Idrissa Sylla, James Perch na Jamie Mackie kwenye majira ya kiangazi. (Mirror)
Mike Ashley atajaribu kwa mara nyingine kuiuza klabu ya Newcastle punde si punde Rafa Benitez atakapomhakikishia kuwa klabu hiyo inabaki Ligi Kuu ya Uingereza na kupewa taarifa ya uwepo wa mnunuaji wa uhakika.
Chaguo la kwanza kwa Arsenal kwenye majira ya joto ni kusajili kiungo wa kati na beki wa kati, huku kukiwa na shaka juu ya hatima ya Jack Wilshere katika klabu hiyo.
Dakatari wa klabu ya Bayern Munich amemtuhumu Pep Guardiola kuwa alikuwa na tabia ya kutokujali afya ya wachezaji wa timu hiyo. (Telegraph)
Jack Wilshere anahofia kwamba ndoto zake kushiriki Kombe la Dunia nchini Urusi zimekufa kwa sababu meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate ana wasiwasi naye.
Isco anatarajiwa kuzigonganisha Manchester City, Chelsea na Tottenham baada ya kukiri kwamba hafurahii kuwa Real Madrid.
FIFA inakabiliana na machafuko juu ya teknelojia ya VAR kwenye Kombe la Dunia kwa sababu waamuzi wengi walioteuliwa kuisimamia tenelojia hiyo hawaitumii kwenye Ligi wazitokea.
James Rodriguez |
James Rodriguez anaweza kuachana na uhamisho kwenda Ligi Kuu ya Uingereza kwa lengo la kubaki Bayern Munich.
Everton wanajipanga kumsajili kiungo wa klabu ya Juventus, Kwadwo Asamoah kwenye majira ya joto. (Sun)
Atletico Madrid wamejiunga na mbio za kuwania saini ya golikipa wa klabu ya Bayer Leverkusen. (Kicker)
Brighton na Aston Villa zina hamu ya kumsajili winga wa timu ya taifa ya Ireland ya Kaskazini, Jordan Jones. (Daily Mail)
Meneja wa West Ham, David Moyes is strongly leaning towards retaining Joe Hart in goal for the crucial match with Southampton.
Danny Cowley na Steve McClaren ndio wagombea wa awali wanaopewa nafasi kubwa kumrithi Mick McCarthy katika klabu ya Ipswich Town. (Times)
Meneja wa Hirbenian, Neil Lennon anasisitiza kwamba John McGinn anaweza kuwa mchezaji tegemezi wa klabu hiyo na kuonya kuwa yeyote atakayemhitaji atalazimika kutoa ofa ya kuanzia pauni milioni 5.
Hearts ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Queen of the South na timu ya taifa ya Australia, Lyndon Dykes. (Record)
Thomas Tuchel |
Aliyekuwa mkufunzi wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel anapewa nafasi kubwa kumrithi Unai Emery katika klabu ya Paris Saint-Germain. (L'Equipe)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 30 Machi, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
3/30/2018 10:45:00 AM
Rating: