Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 3 Machi, 2018

Benzema
Mipango ya rais wa Real Madrid, Florentino Perez kufanya mabadiliko kikosini inaonyesha ni wazi kwamba Karim Benzema amebakiza muda mchache sana katika klabu hiyo. (Don Balon)

Arsene Wenger amepoteza sapoti kutoka bodi ya klabu ya Arsenal baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo dhidi ya Manchester City.

Roy Hodgson anasisitiza kuwa hataisaliti klabu ya Crystal Palace, hata kama atapewa ofa kubwa ya aina yoyote ilele.

Stoke City ina mpango wa kumbakisha Kurt Zouma kwa mkopo kutoka klabu ya Chelsea msimu ujao - kama watabakia Ligi Kuu ya Uingereza. (Sun)

Kiungo wa Real Madrid, Dani Ceballos haijui hatima yake katika klabu hiyo.
Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann atakabidhiwa jezi namba saba kama atakamilisha uhamisho wake kwenda Barcelona. (As)

Alan Pardew amebakiza mechi moja kabla klabu ya West brom haijamfukuza kazi.

Jack Butland amemwomba Gareth Southgate amwambie kama yeye ndiye golikipa namba moja wa Uingereza au la.

Zlatan Ibrahimovic amekiri kuwa ofa ya klabu ya LA Galaxy inamshawishi baada ya kuwa Jose Mourinho amesema anatarajia mshambuliaji huyo wa Sweden ataondoka Manchester United. (Daily Mail)

Ilkay Gundogan
Nyota wa klabu ya Manchester City, Ilkay Gundogan amesema kuwa alikaribia kujiunga na Barcelona kabla hajaamua kwenda Etihad. (Marca)

Pep Guardiola anasema kuwa Manchester City itasajili kati ya mchezaji mmoja au wawili kwenye majira ya joto.

Meneja wa Everton, Sam Allardyce anasisitiza kwamba Michael Keane atarejea kwenye kiwango chake cha siku zote.

Jurgen Klopp anasema kuwa Roberto Firmino anatakiwa aongeze mkataba wake na Liverpool kwa ajili ya mafanikio ya klabu. (Telegraph)

Real Madrid wamejiunga na Barcelona pamoja Manchester United kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya Real Sociedad, Alvaro Odriozola.

Straika wa Chelsea, Eden Hazard na Harry Kane wa Spurs watabakiwa kuwa vinara kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na klabu ya Real Madrid kwenye majira ya joto. (Diario Gol)

Arsene Wenger amewaambia wachezaji wa Arsenal kuwa wako hatarini kuuzwa na klabu hiyo.

Crystal Palace na Newcastle ziko tayari kushindania saini ya golikipa wa klabu ya Burnley, Nick Pope kwenye majira ya joto.

Juventus imemuonya Emre Can kuwa hayuko peke yake kwenye mipango yao baada ya kiungo huyo kuonekana anathamini uhamisho huo. (Mirror)

Scott McTominay anatarajiwa kuipotezea Uskoti na kuamua kuichezea timu ya Taifa ya Uingereza.

Kevin De Bruyne anataka Manchester City itangaze ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuichapa Manchester United Aprili 7. (Star)

Jose Mourinho amemtaka Scott McTominay asiruhusu ushindani uliopo kati ya mataifa mawili juu ya 'future' yake kimtaifa usimpotezee muda. (Express)

Hector Bellerin
Klabu ya Juventus ina mpango wa kumsajili nyota wa Arsenal, Hector Bellerin kwenye majira ya joto. (Guardian)

Mauricio Pochettino anasema kuwa ataondoka Tottenham mara moja kama mashabiki watamgeuka. (Times)

Brenden Rodgers anasisitiza kuwa anaishi maisha ya ndoto zake katika klabu ya Celtic na kuzima uvumi unaodai kwamba atachukua nafasi ya Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal.

Jurgen Klopp ana amini Andy Robertson ana kila sifa za kuchukua nafasi ya Scott Brown kama nahodha wa Uskoti. (Record)

Daktari wa Timu ya Taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar amethibitisha kwamba Neymar atakuwa nje kwa muda wa miezi mitatu baada ya upasujai.

Meneja wa Bayer Municn, Jupp Heynckes amekanusha taariza zinazodai Robert Lewandowsik atajiunga na klabu ya Real Madrid kwenye majira ya joto.

Wakala wa Paul Pogba, Mino Raiola amekanusha taarifa zinazodai kuwa mteja wake hafurahii kuwa Manchester United kwa sababu ya kutoelewa na na Jose Mourinho. (ESPN

Jupp Heynckes
Bayern Munich inatazamia kumpa nafasi meneja wa Freiburg, Christian Streich kukinoa kikosi cha klabu hiyo baada ya Jupp Heynckes kuondoka. (Bild)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 3 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 3 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/03/2018 12:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.