Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 13 Machi, 2018

N'Golo Kante
PSG imeripotiwa kufanya maawasiliano na klabu ya Chelsea juu ya uhamisho wa Thibaut Courtois na N'Golo Kante kwenye majira ya joto.

Meneja wa Juventus, Massimiliano Allegri ndio chaguo la kwanza la klabu ya Arsenal katika makocha inaohitaji wamrithi Arsene Wenger. (Express)

Reus anataka Borussia Dortmund imsajili mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi moja kwa moja.
 
Mark Hughes anapewa nafasi kubwa kuweza kuchukua nafasi ya meneja katika klabu ya Southampton.

Jose Mourinho ameiambia klabu ya Real Madrid isipoteze muda wake kujaribu kumshawishi David de Gea akubaliane na uhamisho kwenda La Liga kwenye majira ya joto. (Sky Sports)

Arsenal iko tayari kumuuza Hector Bellerin kwa pauni milioni 50 kwenye majira ya joto ili kusaidia kuongeza pesa za kufanyia mabadiliko ya kikosi chao.

Alan Pardew atabakia kuwa meneja wa West Brom kufuatia mazungumzo aliyofanya na wakurugenzi wa klabu hiyo. (Daily Mail)

Ousmane Dembele ana miezi mitatu ya kumshawi meneja wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ampe nafasi kwenye kikosi cha timu hiyo kwenye kombe la dunia. 

Paris Saint-Germain wana mpango wa kumrejesha Carlo Ancelotti katika dimba la Parc Des Princes achukue nafasi ya Unai Emery. (L'Equipe

Barcelona imethibitisha kukubaliana na klabu ya Gremio juu ya uhamisho wa Athur Melo kwa takribani pauni milioni 30.

Neymar Jr
Kampuni ya Nike iko tayari kufadhili uhamisho wa Neymar kutoka PSG kwenda Real Madrid kama motisha ya kuwafanya vigogo hao wa La Liga waachane na kampuni ya Adidas. (Marca)

Kiungo wa klabu ya Everton, Gylfi Sigurdsson anaweza kukaa benchi kwa muda wote uliobaki msimu huu. (Telegraph)

Liverpool imepewa matumaini kwenye mbio za kuwania saini ya Stefan De Vrij, huku Inter Milan ikishindwa kuthibitisha kuwa na matarajio ya kumnasa nyota huyo wa Lazio.

Manchester United wanatarajia kurejea sokono kuwinda saini ya Blaise Matuidi mwaka mmoja baada ya kushindwa kufua dafu kwenye usajili wa kiungo huyo wa Ufaransa mbele ya Juventus.

Newcastle wana matumaini ya kumsajili Kenedy moja kwa moja kwenye majira ya joto baada ya nyota huyo ambaye anaichezea klabu hiyo kwa mkopo kutoka Chelsea kuonyesha kiwango kikubwa. (Mirror)

Nyota anayewindwa na Manchester United pamoja na Liverpool, Timo Werner anasema kuwa ataendelea kubakia katika klabu ya RB Leipzig.

Johann Berg Gudmundsson
Leicester, Newcastle na Southampton zinawania waini ya winga wa klabu ya Burnley, Johann Berg Gudmundsson ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 20. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 13 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 13 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/13/2018 12:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.