Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 7 Machi, 2018
Thomas Lemar |
Thomas Lemar anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Anfield akitokea klabu ya Monaco. (Le 10 Sport)
Manchester City bado haijafikia hatua ya kulinagnishwa na Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich, kwa mujibu wa Ilkay Gundogan.
David Luiz amesafiri mara mbili kwenda Barcelona msimu huu kuuonana na mtaalamu wa matatizo ya goti. (Sky Sports)
Mke wa Rais wa Liberia, Clar Weah ameteuliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuwa balozi wa soka ya wanawake.
Buffon anamfananisha mshambuliaji wa klabu ya Tottenham, Harry Kane na aliyekuwa mshambuliaji wa Fiorentina na Timu ya Taifa ya Argentian, Gabriel Batistuta. (ESPN)
Beki wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon angependelea kujiunga na Liverpool kuliko klabu nyingine yoyote ile ya Ligi Kuu ya Uingereza. (Express)
Gianluigi Buffon amesema kuwa alishafanya uamuzi juu ya 'future' yake katika soka - lakini bado hajamwambia meneje wake, Max Allegri kama atabaki au la.
Kiungo wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Uhispania, Dan Caballos anatarajia kuondoka katika klabu yake kwenye majira ya joto baada ya mwaka mmoja tangu ajiunge na vigogo hao wa La Liga. (Corriere dello Sport)
Daley Blind |
Daley Blind anauzwa kuelekea klabu yake ya zamani ya Ajax, huku kukiwa na matarajio kwamba vigogo hao wa Uholanzi wanaweza kushawishika kuachana na Justin Kluivert.
Klabu ya Oxford United iko kwenye mazungumzo na Patrick Kluivert kuhusu kibarua cha kuwa meneja wao mpya.
Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic anatarajia kupata bonasi ya pauni milioni 2 kama klabu yake itawaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Wilfried Zaha ana matumaini ya kurejea katika kikosi cha Crystal Palace siku ya Jumamosi. (Sun)
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane hataki kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane msimu huu. (Diario Gol)
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane hataki kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane msimu huu. (Diario Gol)
Gareth Southgate anatazamia kumjumuisha nyota wa klabu ya Burnley, James Tarkowski kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Uholanziin na Italia. (Telegraph)
Nyota wa klabu ya RB Leipzig, Timo Werner anakiri kuwa na ndoto za kuja kucheza soka katika Ligi Kuu ya Uingereza. (Star)
Manchester United imemjumuisha nyota wa klabu ya Watford, Abdoulaye Doucoure kwenye orodha ya wachezaji ambao inatarajia kuwasajili kwenye majira ya joto.
Eddie Howe |
Bournemouth ina uhakika wa kumbakisha Eddie Howe licha ya kwamba kocha huyo anawaniwa na vilabu kadhaa vyenye majina makubwa.
Bekiwa klabu ya Leicester, Danny Simpson anataka mazungumzo ya haraka na meneja wa klabu hiyo, Claude Puel. (Mirror)
Chelsea inatarajiwa kucheza bila David Luiz kwenye mechi yao ya Ligi ya Kuu dhidi ya Tottenham tarehe 1 Aprili, huku beki huyo akiendelea kukabiliana na benchi kwa mwezi mwingine sasa.
Arsenal inafanya mpango wa kumnasa golikipa wa klabu ya Bayer Leverkusen, Bernd Leno kwa pauni milioni 20 kwenye majira ya joto.
David Alaba ameziweka klabu kubwa za Ulaya kwenye hali ya umakini baada ya kusema kwamba anatazamia kucheza soka nje ya klabu ya Bayern Munich miaka ijayo. (Daily Mail)
Athur Melo |
Mazungumzo juu ya uhamisho wa Athur Melo kutoka Gremio kwenda Barcelona yamegonga mwamba. (Marca)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 7 Machi, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
3/07/2018 01:25:00 PM
Rating: