Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 14 Machi, 2018

Cristiano Ronaldo na Gareth Bale
Ripoti zinadai Cristiano Ronaldo ameshagundua mpango wa Gareth Bale kutaka kutimkia Manchester United kwa dili la uhamisho wa pauni milioni 115.

Romelu Lukaku amewashutumu wachezaji wenzake wa Manchester United kwa kujificha uwanjani wakati wa mchezo wao dhidi ya Sevilla kwenye kombe la Dunia. (Express)

Meneja wa Sevilla, Vincenzo Montella amemwagia sifa Wissa Ben Yedder, mfungaji wa mabao mawili yaliyoitoa Manchester United kwenye Ligi ya Mabingwa.

Barcelona imeachana na mpango wa kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Paris Saint-Germaine, Marco Verrati. (Marca)

Carles Puyol: Eden Hazard bado hajafikia hatua ya kulinganishwa na Lionel Messi.

Winga wa klabu ya Rangers, Daniel Candeias amesaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Uskoti. (Sky Sports)

Klabu Everton inafanya mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere kwenye majira ya joto. (Daily Mail)

Paris Saint-Germain wana mpango wa kutumia pauni milioni 70 kumnasa golikipwa wa klabu ya AC Milan, Gianluigi Donnarumma. (L'Equipe)

Mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig, Timo Werner ndio chaguo la kwanza la Liverpool kwenye majira ya joto.

Arsenal imeripotiwa kufanya mazungumzo na klabu ya Corinthians ya nchini Brazil juu ya uhamisho wa kiungo wa klabu hiyo, Maycon de Andrade.

Jose Luis Gaya
Manchester United ina matumaini ya kuzipiku Arsenal na Chelsea kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa klabu ya Valencia, Jose Luis Gaya.

West Brom inatarajiwa kumbakisha Alan Pardew katika nafasi yake ya kuinoa klabu hiyo hadi mwezi Julai kwa lengo la kuepukana na matumizi fedha nyingi baada ya kumfukuza kazi.

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amembebesha Eden Hazard majukumu yote katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Barcelona. (Mirror)

Harry Kane anaweza kuwa nje ya kikosi cha Tottenham kwa angalau mwezi mmoja au zaidi na kuikosa mechi yao ya muhimu dhidi ya Chelsea.

Mmiliki wa klabu ya PAOK, Savvidis ameomba msamaha kufuatia kitendo cha kuvamia uwanjani akiwa na bastola nchini Ugirirki. (Sun)

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte anatazamia kumwanzisha Olivier Giroud kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona. (Telegraph)

Mark Hughes
Southampton inatazamia kumteuwa Mark Hughes kuwa meneja wao kabla ya mechi yao ya FA Cup dhidi ya Wigan siku ya Jumapili.

Manchester City inaonyesha kukata tamaa kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Shakhtar Donetsk na timu ya taifa ya Brazil, Fred, ambaye anawindwa na Manchester United pamoja na vilabu vingine kadhaa barani Ulaya. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 14 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 14 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/14/2018 12:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.