Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 12 Machi, 2018

Mohamed Salah
Real Madrid watalazimika kulipia kiasi cha pauni milioni 142 kama watahitaji kumnasa winga wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah.

Chelsea iko mstari wa mbele katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid. (talkSport)

Klabu ya West Brom haina mpango wa kuharakisha mpango wa kubadilisha meneja, na badala yake itaendelea kuwa na Alan Pardew.

Nahodha wa klabu ya Atletico Maadrid, Gabi amesema kuwa Antoine Griezmann anatakiwa aendelee kuipa heshima jezi ya klabu hiyo kwa muda wote uliosalia kabla hajaondoka.

Aubaneyang amekiri kuchukizwa na kanuni za UEFA zinazomzuia asishiriki Ligi ya Europa akiwa na Arsenal.

Kiungo wa Manchester United, Scott McTominay ameitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa ya Uskoti kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Costa Rica na Hungary. (Sky Sports)

Baada ya kuifungia timu yake magoli mawili katika mechi yao dhidi ya Udinese, Paulo Dybala anaamini kuwa Juventus ndio mabingwa wa taji la Serie A msimu huu. 

Arturo Vidala anataka Jupp Heynckes aendelea kuwa meneja wa Bayern Munich kwa miaka mingine zaidi ijayo.

Mshambuliaji wa klabu ya Phoenix Rising, Didier Drogba atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu huu. (ESPN

Meneja wa klabu ya Stoke City, Paul Lambert anasema kuwa kitendo cha Pep Guardiola kumkataa Xherdan Shaqiri kimemfanya awe mchezaji bora.

Kurt Zouma
Kurt Zouma anasisitiza kuwa maisha yake katika klabu ya Stoke City ni magumu kuliko alicyokuwa Chelsea.

Arsenal iko tayari kuwaruhusu Eddie Nketiah na Reiss Nelson waondoke katika klabu hito kwa mkopo. (Mirror)

Real Madrid inataka mmoja kati ya Harry Kane, Mohamed Salah, Mauro Icard au Lewandowski achukue nafasi ya mshambuliaji wa klabu hiyo, Karim Benzema kwenye majira ya joto. (Mundo Deportivo)
 
Antonio Conte anasema kuwa Chelsea haina uzoefu wa kuweza kubadilisha matokeo kama Juventus kwenye Ligi ya Mabingwa.

West Ham inahofia adhabu ya kucheza bila mashabiki kwenye uwanja wao kufuatia vurugu za Jumamosi iliyopita. (Daily Mail)

Wamiliki wa klabu ya West Ham wanataka kufanya mabadiliko ya timu nzima ya ulinzi baada ya vurugu zilizotokea Jumamosi.

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte anasema kuwa timu yake lazima ijitese ili kuitoa Barcelona.

Gabriel Jesus ataanza na kikosi cha kwanza cha Manchester City dhidi ya Stoke City, Sergio Aguero akiwa nje baada ya kupata majeraha ya goti. (Telegraph).

Mkurugenzi wa kandanda wa klabu ya Paris Saint-Germain anasema kuwa hana uhakika juu ya 'future' ya Neymar, ambaye kwa sasa anawindwa na klabu ya Real Madrid. (Sun)

Rais wa klabu ya PSG, Nasser Al Khelafi na mkurugenzi wa kandanda wa klabu hiyo, Antero Henrique wanatarajia kwenda Brazil kumuona Neymar.

Paris Saint-Germain inatazamia kusajili kiungo atakayechukua nafasi ya Thiago Motta kwenye majira ya joto. (Telefoot)

Chelsea itakabiliana na ushindani kutoka PSG kama itataka Luis Enrique atue Stamford Bridge.

Jesse Lingard
Jesse Lingard anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu ya Manchester United - miezi 11 ikiwa imepita tangu arekebishiwe mkataba wake wa awali. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 12 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 12 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/12/2018 11:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.