Loading...

Wanaotaka kuandamana waonywa


MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda Simon Sirro, amewataka wazazi na walezi wilayani Kahama, mkoani Shinyanga kuwachunga watoto wao wasitumiwe na viongozi wa kisiasa kushiriki kwenye maandamano yoyote.

Alisema, wanasiasa wanawatumia vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa katika maandamano yasiyokuwa na msingi huku wakitangulizwa mbele na linapotokea varangati wanaoathirika ni vijana hao.

Kamanda Sirro aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kahama, kuwa lengo la ziara yake katika vituo vya polisi hapa nchini ni kufuatilia suala la upelelezi katika kesi ikiwa ni pamoja na kuwakumbuka askari polisi kutenda haki kwa wananchi.

Alisema, asilimia kubwa ya vijana nchini wanatumiwa na viongozi wa kisiasa katika maandamano huku wao wakiwamajumbani kwao ama nyumba yao nakuongeza kuwa kama wazazi hawatalikemea kwa vijana wao suala hili litakuwa sugu katika jamii.

“Wazazi wadhibitini vijana wenu wasitumiwe na viongozi wa kisiasa katika maandamano, kumbukeni vijana wenu ndio nguvu kazi ya taifa kwa miaka ya baadaye…tushirikiane katika kudhibiti wimbi hili na kutoa taarifa za uhalifu katika makazi yetu na tusikubali kubebana katika maovu kisa aliyetenda maovu ni jirani yako,” alisema.
Wanaotaka kuandamana waonywa Wanaotaka kuandamana waonywa Reviewed by Zero Degree on 3/01/2018 11:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.