Loading...

Arusha: Saba wakamatwa kwa kuhamasisha maandamano


Watu saba wamekamatwa kwa uhamasishaji wa maandamano yasiyo halali, yanayotajwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu.

Watu hao wanadaiwa kuhamasisha maandamano hayo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii ya Telegram na Whatsapp.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo, miongoni mwa watuhumiwa hao ni wanafunzi watatu wa vyuo mbalimbali mkoani hapo.

Hata hivyo, Kamanda Ilembo amesita kutaja majina yao amesema ni kwa sababu za kiupelelezi kwani baadhi yao wameshafikishwa mahakamani.
Arusha: Saba wakamatwa kwa kuhamasisha maandamano  Arusha: Saba wakamatwa kwa kuhamasisha maandamano Reviewed by Zero Degree on 4/24/2018 01:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.