Manchester City inaiongoza Arsenal kwenye mbio za kuwania saini ya beki huyu
Licha ya kuongeza nguvu mpya kikosini kwenye majira ya joto mwaka jana, Pep bado ana tamaa ya kuongeza wachezaji wapya kwenye dirisha la usajili linalokuja na ameelekeza macho yake kwa beki wa klabu ya Ajax.
Kwa mujibu wa taarifa ya The Mirror, Manchester City wanapewa nafasi kubwa kuweza kumsajili beki chipukizi wa timu ya taifa ya Uholanzi, Matthijs de Ligt anayeitumikia Ajax. De Ligt anatajwa kuja kuwa kama Virgil van Dijk siku zijazo baada ya kuonyesha ushirikiano mzuri na beki huyo wa kati wa klabu ya Liverpool katika mechi za kimataifa.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18 tayari ameshakataa ofa ya kujiunga na Barcelona kwa sababu anahofia kupigwa benchi. Arsenal na Bayern Munich pia wanamtaka lakini klabu yake inataka pauni milioni 50 kuweza kumruhusu aondoke, kiasi ambacho kinaweza kuwa kimewakatisha tamaa wote na kuiacha nafasi hiyo kwa Manchester City.
Matthijs de Ligt |
Wakati De Ligt alipoulizwa juu ya hatima yake, alisema:
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, klabu zote tatu zilituma maskauti wao kumchunguza De Ligt wakati Ajax ilipokuwa inacheza dhidi ya PSV jana.
“Nitafanya uamuzi kichwani, sio kwa kutazama ofa za fedha.
“Nafikiri wachezaji baadhi wangeweza kushawishiwa na ofa kubwa. Lakini ukilinganisha na watu wa kawaida nadhani ninalipwa mshahara mkubwa kwa sasa.
“Hatua yangu inayofuata inatakiwa iwe sahihi kwangu kwa kuitazama timu iko wapi na ni kwa namna gani nitaweza kuishi.”
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, klabu zote tatu zilituma maskauti wao kumchunguza De Ligt wakati Ajax ilipokuwa inacheza dhidi ya PSV jana.
Manchester City inaiongoza Arsenal kwenye mbio za kuwania saini ya beki huyu
Reviewed by Zero Degree
on
4/16/2018 04:05:00 PM
Rating: