Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 13 Aprili, 2018
Neymar Jr |
Neymar anaweza kuushangaza ulimwengu wa soka kwa kuipotezea ofa ya klabu ya Real Madrid na kuamua kutua Manchester United. (Don Balon)
Fulham imejipanga kumng'ang'ania Ryan Sessegnon licha ya kwamba beki huyo anawindwa na vilabu vingi vwenye uwezo mkubwa kama Tottenham, Liverpool na PSG.
Kiungo wa klabu ya Tottenham, Harry Winks yuko nchini Quatar kwa ajili ya matibabu ya jeraha la kifundo cha mguu.
Mauricio Pochettino anategemea kumrejesha Toby Alderweireld kikosini kabla ya mismu huu kumalizika, hata kama beki huyo anatazamia kuondoka Tottenham kwenye majira ya joto. (Evening Standard)
Manchester United hawana mpango tena wa kumsajili Gareth Bale, ambaye kwa sasa anaweza kuwa njiani kuelekea Inter Milan akitokea Real Madrid kwenye majira ya joto. (Independent)
Tottenham inapanga kumsajili beki wa klabu ya West Ham, Arthur Masuaku kwa pauni milioni 20 mwishoni mwa msimu huu.
Kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko anahitajika katika klabu yake ya zamani, Monaco baada ya kuwa na mwanzo mgumu katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. (Sun)
Arsene Wenger amesema kuwa Danny Welbeck ni mchezaji anayeweza kuiletea Arsenal mafanikio maakubwa, kufuatia goli alilofunga kwenye robo fainali ya Europa Ligi dhidi ya CSKA Moscow.
Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp akiwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Mohamed Salah |
Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp ana uhakika mshambuliaji wa timu hiyo, Mohamed Salah hataondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto kama inavyodaiwa.
Winga wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha amekanusha tuhuma zinazodai kuwa ana tabia ya kujiangusha uwanjani.
Mashabiki wa klabu ya Liverpool wametajwa kuwa vinara wa kupiga kelele uwanjani katika Ligi Kuu ya Uingereza.
Beki wa klabu ya Rangers, David Bates ataondoka kwenda Hamburg kwenye majira ya joto baada ya kukubali mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya Ujerumani. (Sky Sports)
Chelsea wanamchunguza nyota kutoka Brazil anayewindwa na klabu ya Man City, Eder Militao kuelekea mpango wao wa mabadiliko makubwa Stamford Bridge.
Meneja wa klabu ya Napoli, Maurizio Sarri ametajwa miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Antonio Conte katika klabu ya Chelsea.
Beki na nahodha wa West Brom, Jonny Evans ataachana na uhamisho kwenda Arsenal na anaweza kuchagua kujiunga na Manchester City.
Mkufunzi mkuu wa Eintracht Frankfurt, Niko Kovac anatarajiwa kutangazwa kama meneja mpya wa klabu ya Bayern Munich.
Dusan Tadic |
Klabu ya A.S Roma inamtaka winga wa Southampton, Dusan Tadic. (Mirror)
Viongozi wa Ligi Kuu ya Uingereza wanatarajiwa kurudisha nyuma utambulisho wa Teknolojia ya VAR kwa mwaka mmoja kwenye mkutano wa Ijumaa lakini wataruhusu majaribio katima msimu wa 2018-19.
Inawezekana kuwa Saido Berahino amecheza mechi yake ya mwisho katika klabu ya Stoke City msimu huu baada ya meneja wa klabu hiyo, Paul Lambert kumsimamisha mshambuliaji huyo kwa kukosa maadili. (Telegraph)
Paris Saint-Germain wameanza mazungumzo na golikipa wa klabu ya Chelsea, Thibaut Courtois juu ya uhamisho wake kwenda Ligue 1 kwenye majira ya joto.
Kiungo anayeichezea klabu ya Crystal Palace kwa mkpo kutoka Chelsea, Ruben Loftus-Cheek anaamini anaweza kujumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia kama ataepukana na majeruhi hadi mwisho wa mismu. (Daily Mail)
Rafa Benitez anaamini kuwa Newcastle inaweza kukabiliana na Chelsea pamoja na Tottenham kumbakisha beki na nahodha wa klabu hiyo, Jamaal Lascelles.
Klabu ya Notts County inamtaka Joey Barton, ambaye kifungo chake cha miezi 14 kutokana na kukiuka masharti ya michezo ya bahati nasibu kinaisha tarehe 1 mwezi Juni. (Star)
Aleksandar Mitrovic ameiambia klabu ya Fulham kuwa inatakiwa kuhakikisha meneja wake, Slavisa Jokanovic haondoki. (Express)
Steven MacLean |
Hearts wanategemea kumnasa mshambuliaji wa klabu ya St Johnstone, Steven MacLean. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 13 Aprili, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
4/13/2018 10:05:00 AM
Rating: