Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 27 Aprili, 2018

David de Gea
Jose Mourinho amesema kuwa hakuna uwezekano kwa golikipa wa klabu hiyo, David de Gea kuondoka kwenye majira ya joto.

FIFA yamfungia Rais wa Shirikisho la Soka nchini Brazil, Marco Polo Del Nero baada kukutwa na hatia ya kupokea rushwa.

Sam Allardayce anasema kuwa hataondoka Everton na ameshanza kupanga mikakati ya msimu ujao na bosi wa klabu hiyo, Farhad Moshiri. (Sky Sports)

Luis Enrique anataka pauni milioni 200 kufanya mabadiliko makubwa Arsenal... na washambuliaji pekee ndio wenye uhakika wa kusalia katika kikosi cha klabu hiyo.

Jose Mourinho anailaumu Chelsea kwa kumuuza Mohamed Salah - na anasema kuwa the Blues walisema uongo kuhusiana na kuondoka kwa nyota huyo.

Arsenal itakabiliana na Atletico Madrid pamoja na Napoli kumsajili golikipa wa Bayer Leverkusen, Bernd Leno anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 17.5. (Sun)

Jonny Evans
West Ham imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa West Brom, Jonny Evans anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 3, huku klabu hiyo ya Uingereza ikijiandaa kushuka daraja.

Roman Abramovich amewaagiza wakurugenzi wa klabu ya Chelsea kuandaa mipango ya usajili, licha ya kutokuwepo na uhakika wa Antonio Conte kuendelea na kibarua chake.

Kiungo wa klabu ya Roma, Radja Nainggolan amesistiza kuwa kilichoitokea Barcelona kinaweza kikajirudia kwenye Ligi ya Mabingwa - safari hii ikiwa ni dhidi ya Liverpool.

Meneja wa Leicester City, Claude Puel amesifia uwezo wa Jamie Vardy kama nahodha wa klabu hiyo. (Mirror)

Steven Gerrard anatarajia kumteua Gary McAllister kuwa msaidizi wake kwenye kibarua chake kipya kama meneja wa Rangers.

Hatima ya Sam Allardyce katika klabu ya Everton iko shakani baada Farhad Moshiri kuacha kumuunga mkono.

Claude Puel
Claude Puel anakabiliwa na hatari ya kutimuliwa Leicester, huku kukiwa na shaka juu ya uwezo wake wa kufanya mabadiliko katika klabu hiyo kwenye majira ya joto.

Tottenham wanajiandaa kuingiza karibu pauni milioni 170 kwa kuwauza nyota wao wa kikosi cha kwanza - Danny Rose, Toby Alderweireld, Victor Wanyama pamoja na Mousa Dembele kwenye majira ya joto. (Daily Mail)

Klabu ya Ipswich Town itafanya mahojiano na Sol Campbell, katika mwendelezo wa msako wa meneja mpya.

Claude Puel anapigana kuokoa kibarua chake kama meneja wa Leicester City, kuelekea mabadiliko makubwa katika klabu hiyo kwenye usajili wa majira ya joto. (Telegraph)

Alexis Sanchez ataongeza nguvu ya kuifunga Arsenal wakati Manchester United itakapokabiliana na timu hiyo Jumapili, kwa mujibu wa Phil Jones. (Express)

Golikipa wa zamani wa Liverpool, Ray Clemence ameishauri klabu hiyo kumsajili Jack Butland kutoka Stoke City kwenye majira ya joto.

Hector Bellerin
Barcelona wako tayari kumtoa Ousmane Dembele kama sehemu ya ofa yao kumnasa Hector Bellerin kutoka Arsenal kwenye majira ya joto. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 27 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 27 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/27/2018 11:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.