Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 14 Aprili, 2018

Antonio Conte akiwa na baadhi ya wachezaji wa Chelsea
Marcel Desailly amesema kuwa Chelsea inatakiwa kumbakisha Antonio Conte na badala yake iwauze wachezaji wake waliocheza chini ya kiwango msimu huu.

Ander Herera amesema kuwa hajui kama ataongeza mkataba wake katika klabu ya Manchester United.

Diego Costa anaweza kuukosa mchezo wa kwanza wa Atletico Madrid dhidi ya Arsenal kwenye Ligi ya Europa. (ESPN)

Aliyekuwa mkufunzi wa Sevilla, Eduardo Berizzo atachukua nafasi ya Jose Angel Ziganda kama meneja wa Athletic Bilbao kwenye majira ya joto. (Marca)

Barcelona wanatarajia mwezi huu Andres Iniesta atawaambia kama ataondoka kwenda China mwishoni msimu huu. (Mundo Deportivo)

Oliver Giroud anasema kuwa ilikuwa jambo rahisi kwake kuamua kuondoka Arsenal kwenda Chelsea kwa sababu 'ni timu bora Uingereza'.
 
Pep Guardiola anasema kuwa Manchester United bado ina nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza.

Antonio Conte amekiri kwamba ni vigumu kwa Chelsea kumaliza Ligi Kuu katika nafasi nne bora.

Niko Kovac
Niko Kovac anarejea Bayer Munich kama mkufunzi mkuu wa klabu hiyo msimu ujao, baada ya kufanya vizuri akiwa na Eintracht Frankfurt. (Sky Sports)

Manchester United ina nia ya kumsajili beki kutoka klabu ya Partizan, Svetozar Markovic.

Manchester United imemchukua golikipa chipukizi kutoka Slovenia, Zan-Luck Leban kwa ajili ya majaribio. (Manchester Evening News)

West Ham wanatafakari juu ya kujaribu kumsajili kiungo wa klabu ya Chelsea, Danny Drinkwater, ambaye amekuwa na wakati mgumu tangu atue Stamford Bridge.

Liverpool wana mpango wa kumrejesha Suso kutoka AC Milan kwa pauni milioni 35, miaka mitatu ikiwa imepita tangu aondoke Anfield kama mchezaji huru.

Mashabiki wanaamini kuwa Droo ya Ligi ya Mabingwa ilipangwa kabla kufuatia Roma kutangaza ticketi za mechi yao dhidi ya Liverpool kabla ya kufanyika kwa droo hiyo.

Jay Rodriguez ameapa kuwa atapigana vilivyo kusafisha jina lake - licha ya FA kwa ubaguzi.

Alexandre Lacazette anakazania kupata heshima ya Europa Ligi - ili Arsene Wenger aendelee kubaki Arsenal. (Sun)

Kieran Tierney
Jose Mourinho ametuma maskauti wa Manchester United kumchunguza beki wa klabu ya Celtic, Kieran Tierney kwenye mechi yao dhidi ya Rangers wikendi hii.

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp anasema ataangalia mikanda ya video ya mechi za klabu hiyo za Ligi ya Mabingwa kuelekea mchezo wao wa nusu fainali ya michuano hiyo dhidi ya Roma. (Daily Mail)

Joe Cole amesema kuwa anataka kurejea Chelsea siku za mbeleni na kuwa sehemu ya benchi la ufindi la klabu hiyo. (London Evening Standard)

Beki wa Barcelona, Samuel Umtiti amewauzi waamuzi wa klabu hiyo pamoja na Manchester United kwa kufanya mazungumzo ya siri na Real Madrid. (Express)

Michael Carrick alifanya mazungumzo na wachezaji wa Manchester United wakati wa mapumziko katika Uwanja wa Etihad yaliyowahamasisha kurejea mchezoni kwa kurudisha magoli mawili waliyofungwa kipindi cha kwanza.

Kiungo wa klabu ya Roma, Daniele De Rossi amekiri kuwa alifikiri Manchester City ingeifunga Liverpool - na kwamba kwa sasa 'anawazimu' juu ya mkufunzi wa Liverpool, Jurgen Klopp. (Mirror)

Klabu ya MLS, DC United inataka kumsajili mshambuliaji wa West Ham, Javier Hernandez, ambaye hafurahishwi na kuanzia benchi chini ya utawala wa David Moyes. (Star)

Arsene Wenger anategemewa kuendelea kuinoa Arsenal msimu ujao kama the Gunners watafanikiwa kutinga fainali ya Ligi ya Europa.

Teknolojia ya VAR haitatumika kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao
Pep Guardiola amezituhumu Manchester United na Chelsea kuwa miongoni mwa klabu zinazozuia kuanza kutumika kwa Teknelojia ya VAR katika Ligi Kuu ya Uingereza. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 14 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 14 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/14/2018 10:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.