Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 17 Aprili, 2018

Arturo Vidal
Kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal anaweza kuikosa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid kutokana na majeraha.

Fernando Torres amesema kuwa hataendelea kucheza soka nchini Uhispania, huku akiwa kwenye maandalizi ya kuondoka Atletico Madrid.
  
Graham Hunter anaamini kuwa Real Madrid inampaango wa kumuuza Gareth Bale baada ya kumwacha nyota huyo nje ya kikosi kilichoibuka kidedea dhidi ya Malaga.

Michy Batshuayi anatarajiwa kukosa mechi zote za msimu huu katika klabu ya Borussia Dortmund zilizobaki na anaweza kukosa Kombe la Dunia kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu. (Sky Sports)

Straika wa klabu ya West Ham, Javier Hernandez anaweza kutimukia nchini marekani kwenye majira ya joto.
Aliyekuwa nyota wa zamani wa Liverpool, Danny Murphy anasema kuwa Rafa Benitezi ni kocha mzuri na anafaa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal. (talkSport)

Mkufunzi wa klabu ya Barcelona amesema kuwa timu ya taifa ya Argentina haitakiwa kuwa na hofu juu ya hali ya Lionel Messi.

Golikipa wa Misri, Ahmed El Shenawy atakosa Kombe la Dunia baada ya kuumia goti wiki iliyopita. (ESPN)
  
Pep Guardiola
Manchester City itafanya mazungumzo na Pep Guardiola kujaribu kumshawishi Mhispania huyo aongeze mkataba wake hadi mwaka 2020.

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino anataka kukamilisha mikakati yote ya uhamisho kabla Kombe la Dunia halijaanza.

Klabu kubwa za Ligi Kuu ya Uingereza zinaweza kutakiwa kulipa kodi kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho klabu hizo zinapokea kutoka katika mikataba na Televisheni mbalimbali. (Times)

Manchester City inaendelea kusubirishwa katika hali ya wasiwasi juu ya uwezekano wa kufungiwa usajili kutokana na kesi ya Benjamin Garre.

Manchester United wanatarajiwa kuwaacha Alexis Sanchez na Paul Pogba nje ya kikosi kitakachocheza mechi ya nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Tottenham.

Trent Alexander-Arnold anatarajiwa kusaini kandarasi mpya katika klabu ya Liverpool. (Telegraph)

Wachezaji wa Manchester City wanatarajia kupata bonasi ya pauni milioni 10 mwishoni mwa msimu huu.

Arsene Wenger anaweza kupoteza kibarua chake mwishoni mwa msimu huu kwa sababu ya kupungua kwa mashabiki wanaoingia Emirates. (Daily Mail)

Ivan Rakitic
Ivan Rakitic yuko tayari kwa uhamisho kwenda Old Trafford, huku akiwa na hofu kuwa vinara hao wa La Liga wako kwenye msako wa mtu atakayechukua nafasi yake.

Arsenal ndio vinara kwenye mbio za kuwania saini ya chipukizi wa klabu ya Barcelona, Robert Navarro.

Liverpool inakabiliana na Barcelona kumsajili nyota mwenye asili ya Kifaransa anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 39, Clement Lenglet kutoka Sevilla, huku mazungumzo yakitarajiwa kuanza wikendi hii.

Meneja wa Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Uingereza (Man City), Pep Guardiola atapewa pauni milioni 200 kama kianzio kwenye usajili wa majira ya joto.

Tottenham imewataja Bryan Cristante na Andre Gomes kama wagombea sahihi wa nafasi ya Mousa Dembele. (Mirror)

Marcus Rashford atachelewesha uamuzi wake wa kusaini mkataba mpya katika klabu ya Man Utd baada ya kupoteza nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha wkanza cha klabu hiyo.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anatarajiwa kurejea sokoni kuwania saini ya kiungo wa Napoli, Piotr Zielenski kwa mara nyingine baada ya kushindwa kumnasa nyota huyo mwaka 2016.

Philippe Coutinho atarejea Anfield kwenye majira ya joto katika mchezo wa maandalizi ya Kombe la Dunia kati ya Brazil na Croatia.

Viktor Claesson
Swansea wanalenga kumsajili kiungo wa Sweeden anayichezea klabu ya Krasnodar, Viktor Claesson kwenye majira ya joto. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 17 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 17 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/17/2018 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.