Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 24 Aprili, 2018


Beki wa klabu ya Juventus, Alex Sandro ni kinara kwenye orodha ya wachezaji ambao Paris Saint-Germain inawahitaji. (Le10Sport)

Inter Milan inamtaka kiungo mshambuliaji wa klabu ya Villarreal, Roberto Soriano.

Meneja wa Barcelona, Ernesto Valverde anaweza kuondoka katika klabu hiyo licha ya kutwaa vikombe viwili. (Diario AS)

Meneja mpya wa Arsenal atapangiwa bajeti ya pauni milioni 50 pekee kwenye usajili wa majira ya joto.

Kwa mujibu wa aliyekuwa golikipa wa klabu ya Newcastle, Shay Given, Liverpool itafanikiwa kumbakisha Mohamed Salah Anfield.

Leicester City ina nia ya kumsajili beki wa kulia wa klabu ya Porto, Ricardo Pereira.

Beki wa klabu ya Middlesbrough, Dael Fry amesaini kandarasi mpya ya miaka mitano.

Carlo Ancelotti amepewa ofa ya kuinoa timu ya taifa ya Italia. (Sky Sports)

John McGinn anasema kuwa anaipenda klabu ya Hibernian lakini anataka ajaribu uwezo wake katika ngazi za juu. (Telegraph)

Klabu ya Manchester City wako tayari kumuuza beki wao, John Stones kwenye majira ya joto.

Glen Kamara
Swansea itazikabili Celtic pamoja Rangers kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Dundee, Glen Kamara kwenye majira ya joto.

Sir Alex Ferguson alitaka kuwasajili Ilkay Gundogan, Mats Hummels na Marco Reus kabla ya kutangaza kuondoka Manchester United mwaka 2013.

RB Leipzig walijaribu kumsajili Trent Alexander-Arnold mwezi Januari wakati Liverpool ilipojaribu kupeleka ofa ya kumsajili Naby Keita. (Sun)

Danny Rose anabakia kuwa kwenye mipango ya usajili ya Manchester United licha ya kuachwa benchi sana katika klabu ya Tottenham msimu huu.

Declan Rice atapewa ofa ya kandarasi mpya West Ham. (Evening Standard)
 
Paul Pogba anasistiza kwamba Jose Mourinho hana shida na mtindo wake wa nywele baada ya maoni yaliyotolewa na meneja huyo wa Manchester United hivi karibuni. (Times)

Alexis Sanchez anasema kuwa Jose Mourinho alimwambia huwa hapendelei kusajili wachezaji mwezi Januari na hategemei kama ataweza kuendana na matakwa yake kwa muda mfupi.

Dani Alves amefungua milango kwa uhamisho wa kushitukiza kurejea katika klabu ya Barcelona. (Express)

Manchester City ilifanya mazungumzo na wakala wa kiungo wa klabu ya Napoli,  Jorginho licha ya nyota huyo kuhusishwa sana na klabu ya Liverpool.

Mkufunzi wa klabu ya Barcelona, Ernesto Valverde anatafakari juu ya hatima yake katika klabu hiyo licha ya kubakiwa na siku chache kushinda mataji mawili katika msimu wake wa kwanza. (Daily Mail)

Marouane Fellaini 
Kiungo wa Manchester United, Marouane Fellaini tayari ameshawasiliana na Paris Saint-Germain, Juventus, Monaco, Besiktas, West Ham na Leicester kuelekea dirisha la usajili wa majira ya joto.

Mshambuliaji wa LA Galaxy, Zlatan Ibrahimovic anasema kuwa anataka kuingia kwenye Uigizaji Hollywood baada ya kustaafu soka.

Mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig, Emil Forsberg ameiwashia Arsenal taa ya kijani baada ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa anaondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani.

Beki wa Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani, Shkodran Mustafi anasistiza kwamba anataka kusalia katika klabu hiyo baada ya Arsene Wenger kuondoka licha ya mashabiki pamoja na vyombo vya habari kukosoa kiwango chake msimu huu.

Kiungo wa Liverpool, Lazar Markovic amekasirishwa na kitendo cha klabu hiyo kutaka kumuuza kwa bei kubwa licha ya kutopata muda wa kutosha kuitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka mitatu.

Fernando Llorente yuko tayari kuondoka katika klabu ya Tottenham kwenye majira ya joto. (Mirror)

Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Arsenal, Peter Hill-Wood anasema kuwa Arsene Wenger, ambaye yeye ndiye alimleta London Kaskazini, alikuwa sahihi kuamua kuodnoka.

Kitendo cha Lionel Messi kukataa kukubaliana na mpango wa Barcelona kumsajili Antoine Griezmann kinaipa Manchester United nafasi ya kumsajili Mfaransa huyo. (Star)

Olivier Giroud 
Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Olivier Giroud aliwaambia wachezaji wenzake kwamba Uwanja wa Wembley ni 'bustani' yake kwa sababu hana rekodi ya kufungwa pale. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 24 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 24 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/24/2018 11:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.