Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 1 Aprili, 2018

Paulo Dybala
Kocha wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone anasema kuwa hakupanga kukutana na Paulo Dybala wiki hii.

Barcelona inatarajia kumkaribisha Sergio Busquets mazoezini Jumatatu na nyota huyo wa Uhispania anatarajiwa kuwa fit kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma Jumatano. (AS)
 
Real Madrid wanaweza kumpa Alvaro Morata nafasi ya kurejea Bernabeu kutoka Stamford Bridge kwenye majira ya kiangazi.

Liverpool imepata ahueni baada ya klabu ya Real Madrid na Barcelona kujitoa kwenye mbio za kuwania saini ya Mohamed Salah.

Arsenal wanaimarisha ulinzi na usalama wakati mashabiki wa CSKA Moscow wakijiandaa na michuano ya Europa Ligi. (Express)

Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich, Karl- Heinz Rummenigge anasema kuwa klabu hiyo atateuwa na kutanga kocha mpya mwisho wa mwezi huu.

Mchezaji anayewindwa na klabu ya Arsenal, Bernd Leno amekataa kusaini mkata mpya na klabu yake ya Bayer Leverkusen.
  
Eljif Elmas
Borussia Dortmund inatarajiwa kukabiliana na Manchester City, Feyenoord na PSV kuwania saini ya nyota wa klabu ya Fernabache, Eljif Elmas. (Bild)

Paul Pogba anasisitiza kwamba hakuna tofauti zozote kati yake yeye na kocha Jose Mourinho. (Sky Sports)

Manchester United watamtoa sadaka Anthony Martial kwa lengo la kudhamini uhamisho wa Gareth Bale kwenye majira ya joto.

Chelsea wanapanga kumsajili nyota wa klabu ya Newcastle, Jamaal Lascelles kwa pauni milioni 30 aje kuwa John Terry kwenye majira ya kiangazi.

Uingereza inatarjiwa kumtema Joe Hart kwenye fainali za Kombe la Dunia  baada ya miaka mingi kama golikipa namba moja wa taifa hilo.

Arsenal wanamfuatilia kwa karibu chipukizi wa klabu ya Ajax, Matthijs de Ligt.

Alan Hutton anahitajika katika klabu ya Middlesbrough na Ipswich wakati atakapoondoka Aston Villa kwenye majira ya joto.

Nyota wa Celtic, Kristoffer Ajer ameivutia klabu ya Borussia Dortmund. (Mirror)

Manchester United wanatazamia kuajiri safu mpya ya ulinzi kama sehemu ya mpango wao wa kufanya mabadiliko ya kikosi chao kwenye majira ya joto, huku beki wa Barcelona, Samuel Umtiti na Juventus, Alex Sandro wakiwa miongoni mwa wachezaji wanaohitajika kwa sana katika klabu hiyo. (Times)

Ndoto ya Adam Lallana kushiriki Kombe la Dunia iko shakani baada ya nyota huyo kupata majeraha ya mguu katika dimba la Selhurst.

Beki wa klabu ya Crystal Palace, Pape Souare amefiliisika licha ya kulipwa pauni 30,000 kwa wiki katika klabu hiyo ya Uingereza.

Antonio Conte amekiri kwa mara ya kwanza kuwa hana uhakika kama atakuwa meneja wa Chelsea msimu ujao.

Vincent Kompany anakiri kwamba, kama watatangaza ubingwa wa Ligi Kuu katika mechi dhidi ya mahasimu wao wakubwa, Man United itakuwa na maana kubwa sana kwa mashabiki wa Man City. (Daily Mail)

Wilfred Ndidi
Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa klabu ya Leicester City, Wilfred Ndidi.

Antoine Griezmann amepotezea uhamisho wake kwenda Manchester United na kukubali uhamisho wa pauni milioni 88 kwenda Barcelona.

Arsenal hawana kasi ya kukazania mazungumzo ya mkataba mpya na Jack Wilshere - kutokana na kwamba hakuna vilabu vinavyoonyesha juhudi ya kutaka kumsajili waia huyo wa Uingereza.

Alan Pardew anaweza kuendelea kuinoa West Brom hata kama klabu hiyo itashuka daraja.

Crystal Palace wamweka mstari wa mbele nyota wa klabu ya Everton, Ademola Lookman kwenye orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kumrithi Wilfried Zaha - ambaye anahusishwa na uhamisho kwenda vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Uingereza kwenye majira ya joto.

Southampton inatazamia kumuuza golikipa wa klabu hiyo, Fraser Forster kwa mkopo msimu ujao.

Max Meyer
Arsenal na Liverpool zimekaa mkao wa kula baada ya klabu ya Schalke 04 kuthibitisha kuwa Max Meyer ataondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya kiangazi. (Sun)

Arsenal imeripotiwa kupeleka ofa Real Madrid kwa ajili ya kumnasa golikipa wa klabu hiyo, Keylor Navas achukue nafasi ya Petr Cech.

Marcus Rashford anaweza kutumika kama sehemu ya makubaliano kwa Jose Mourinho kumnasa nyota wa Real Madrid, Isco. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 1 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 1 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/01/2018 10:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.