Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 15 Aprili, 2018

Andres Iniesta
Nahodha wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta amesema kuwa ataamua juu ya hatima yake katika klabu hiyo na atatangaza uamuzi wake kama atabaki Nou Camp au la kabla ya mwisho wa mwezi huu. (Sport)

Winga wa klabu ya Bordeaux, Malcom amesema anatamani sana kujiunga na Paris St-Germain. (Le10Sport)

Liverpool wana mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Poland, Piotr Zielinski.

Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne amekiri kwamba Mohamed Salah anastahili kupewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka (PFA).

Oliver Giroud anasema kuwa Chelsea haitakata tamaa kupigania kumaliza Ligi Kuu katika nafasi nne bora.

Mshambukliaji wa Swansea, Jordan Ayew ana uhakika klabu yake haitashuka daraja msimu huu.

Nahodha wa Newcastle, Jamaal Lascelles amesema kuwa Rafa Benitez ni kocha wa kipekee. (Sky Sports)

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola ana mpango wa kumnasa kiungo wa Bayern Munich, Thiago Alcantara kwa pauni milioni 50.

Danny Welbeck
Arsene Wenger amesema kuwa Danny Welbeck anastahili kupewa nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia.

Golikipa wa klabu ya Juventus, Gianluigi Buffon amekataa kumuomba msamaha mwamuzi Michael Oliver kufuatia timu yake kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa katika mazingira yenye utata wiki hii. (Daily Mail)

Manchester City wanatazamia kumsajili Kylian Mbappe kama nyota huyo atalazimishwa kuondoka Paris Saint-Germain.

Manchester City wanapewa nafasi kubwa ya kuweza kumnasa chipukizi wa klabu ya Ajax, Matthijs de Ligt dhidi ya Arsenal.

Manchester United wanafanya mchakato wa kumsajili beki kutoka Leicester, Harry Maguire kwenye majira ya joto.

Eliaquim Mangala ataigharimu Manchester City karibu pauni milioni 1 kwa kila mechi moja wakati atakapoondoka kwenye majira ya joto.

Liverpool wanatarajiwa kumpa beki wao, Trent Alexander-Arnold ofa ya mkataba mpya baada ya kuwa na msimu mzuri Anfield.

Mmiliki wa klabu ya Everton, Farhad Moshiri anamleta wakala mzoefu, Mino Raiola kuandaa mchakato mzima wa mabadiliko ya kikosi cha klabu hiyo.

Jose Mourinho
Jose Mourinho anasisitiza kuwa Manchester United haitakuwa na matumizi makubwa yasiyokuwa na tija kwenye majira ya joto. (Mirror)

Liverpool wanatarajia kumsajili binamu yake na Steven Gerrard, Bobby Duncan kutoka Manchester City.

Steven Gerrard ameibuka na kuwa kinara wa wagombea wa nafasi ya meneja katika klabu ya Ipswich.

West Ham wanaisaka saini ya straika wa klabu ya Nice, Alassane Plea - lakini watalazimika kulipa pauni milioni 25 kumnasa Mfaransa huyo.

Manchester United wataikabili Liverpool tarehe 28 Julai kwenye michuano ya Mabingwa ya Kimataifa (International Champions Cup).

Meneja wa Juventus, Massimiliano Allegri ameanza kujifunza Kiingereza, huku kuwa na tetesi zinazodai ana mpango wa kujiunga na Ligi Kuu ya Uingereza.

Everton walimtuma skauti wao kumchunguza beki wa Colombia, Frank Fabra, ikiwa ni sehemu ya mpango wao wa kumnasa nyota huyo. (Sun)

Brendan Rodgers yuko kwenye orodha ya watu wanne wanaotarajiwa kurejea kwenye Uingereza kuchukua nafasi ya Antonio Conte kama meneja mpya wa Chelsea. (Express)

Robert Lewandowski 
Chelsea wako kwenye tahadhari baada ya mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski kuwekwa sokoni. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 15 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 15 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/15/2018 12:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.