Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 22 Aprili, 2018

Cristiano Ronaldo
Real Madrid wanatarajia kumpa Cristiano Ronaldo ofa ya mkataba mpya. Wakati mkataba wake wa sasa ambao utaisha mwaka 2021 hautaongezwa, mshahara wake utaongezwa kutoka pauni milioni 18.42 hadi 26.32 kwa mwaka. (AS)

PSG wanahofia Neymar yuko anafanya mipango ya kutimkia Real Madrid kwenye majira ya joto. (Marca)

Borussia Dortmund wanatafakari juu ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Michy Batshuayi kwa mkataba wa kudumu kwenye majira ya joto.
 
Mshambuliaji wa Bayern Munich anabikia kuwa na tamaa ya kujiunga na Real Madrid kwenye majira ya joto. (Bild)

PSG inakabiliana na ushindani kutoka Napoli kwenye mbio za kuwania saini ya golikipa wa Sporting, Rui Partricio. (Le10Sport)

Kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho anapendelea kujiunga na Manchester City badala ya Manchester Unitde. (ESPN)
 
Antonio Conte anaamini itakuwa ni vigumu kushinda taji la FA Cup msimu huu baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kushinda taji hilo msimu uliopita.

Arsene Wenger anasema kuwa Shkodran Mustafi anaadamwa na kutojiamini kwa sasa.

Arsene Wenger
David Moyes anaamini kwamba meneja wa Arsenal, Arsene Wenger atawindwa na mataifa mengi baada ya Kombe la Dunia kwa lengo la kumpa kibarua cha ukufunzi. (Sky Sports)

Arsene Wenger anatarajiwa kupewa ofa ya nafasi ya kujiunga na PSG - kama rais wa klabu hiyo ya Ufaransa, huku Thomas Tuchel akiwa kama mkufunzi mkuu wa klabu hiyo.

Chelsea inachelewesha kuondoka kwa Antonio Conte kwa sababu klabu hiyo italazimika kumlipa kiasi cha pauni milioni 10 kama itaamua kumfukuza kazi.

Marouane Fellaini anawaniwa na vilabu zaidi ya sita, PSG, Juventus na West Ham ikiwa ni miongoni mwa klabu hizo.

Max Allegri, Leonardo Jardim na Brendan Rodgers wanaweza kufanya mazungumzo na klabu ya Arsenal juu ya nafasi ya Arsene Wenger.

Uteuzi wa Marcel Brand kuwa Mkurugenzi wa Kandanda katika klabu ya Everton unatarajiwa kutangazwa, huku winga wa klabu ya PSV, Hirving Lozano akipewa nafasi ya kuwa mchezaji wa kwanza atakayesajiliwa na mkurugenzi huyo.

Watford haitamzuia Richarlison kuondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto endapo itatokea klabu ambayo itakuwa tayari kulipa kiasi cha pauni milioni 40. (Mirror)

Arsenal inatarajia kuikabili Chelsea kuwania saini ya Max Allegri, huku  Arsene Wenger akilengwa na klabu ya PSG.

Jamie Vardy 
Pep Guardiola anataka kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Manchester City kilichotwaa Taji la EPL kwa kuwasajili Thiago Alcantara na Jorginho kwa jumla ya pauni milioni 135 kwenye majira ya joto. (Star)

Newcastle wamekataa ofa ya pauni milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji wa klabu hiyo, Aleksandar Mitrovic, ambaye ameonyesha uwezo wa kuvutia akiwa na Fulham kwa mkopo.

Jack Grealish atasalia Aston Villa msimu ujao hata kama klabu hiyo haitapanda daraja.

Mshambuliaji wa Rubin Kazan, Sardar Azmoun anawindwa na Everton, Leicester City, Wolves pamoja na Celtic.

Fulham wataikabili West Ham kumbakisha beki wao, Ryan Fredericks, ambaye atakuwa mchezaji huru kwenye majira ya joto. (Sunday People)

Arsenal wamezungumza na Luis Enrique kuhusiana na kuchukua nafasi ya Arsene Wenger, huku Max Allegri na Brendan Rodgers wakiwa kwenye rada ya the Gunners.

Arsene Wenger alilipwa pauni milioni 11 ili aachie ngazi katika klabu ya Arsenal mwaka mmoja kabla, klabu hiyo ilipokuwa na shauku kubwa ya kurejea Ligi ya Mabingwa.

Kufuatia tangazo lake la kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu, Arsene Wenger anatarajiwa kuanza mazungumzo na PSG pamoja na klabu yake ya zamani, Monaco.

Jamie Vardy 
Jamie Vardy atapewa ofa ya mshahara wa pauni 140,000 kwa wiki ili asalie Leicester na kuongeza mkataba wake, ambapo kwa sasa amebakiwa na miaka miwili ya kuitumikia klabu hiyo.

Meneja wa Newcastle, Rafa Benitez ameupa kipaumbele usajili wa straika mpya kwenye majira ya joto, huku nyota wa klabu ya Bournemouth, Josh King akiwa chaguo lake la kwanza.

Manchester United wamemuongeza beki wa kati wa klabu ya Sevilla, Clement Lenglet kwenye orodha ya wachezaji wanaowahitaji kwenye usajili wa majira ya joto lakini watakabiliana na ushindani kutoka Barcelona kumnasa nyota huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa U21.

Kiungo wa Brighton, Pascal Gross anahitajika katika klabu ya RB Leipzig, ambayo meneja wake, Ralf Rangnick alikuwa Hoffenheim wakati kiwango cha nyota kilipoanza kukua.

Swansea City wanatarajiwa kujaribu kumshawishi Oli McBurnie, ambaye ameonyesha kiwango cha kuvutia akiwa Barnsley kwa mkopo asalie klabuni kwa kumuongezea mshahara, huku kukiwa na tetesi zinazohmusisha na uhamisho kwenda Leeds, Derby na Reading.

Kiungo wa Sunderland, George Honeyman anaweza kushawishika na uhamisho kwenda Sheffield Wednesday baada ya klabu hiyo kushushwa daraja Jumamosi iliyopita. (Sun)

Jose Mourinho hatamzuia Anthony Martial kuondoka kama straika huyo ataamua kuachana na Manchester United kwenye majira ya joto.

Njia ya Arsenal kumfanya Luis Enrique kuwa meneja wao mpya ni nyeupe baada ya Chelsea kupunguza kasi ya kuwania saini ya Mhispania huyo. (Times)

Ryan Sessegnon
PSG wana uhakika wa kuipiku Manchester United kwenye mbio za kuwania saini ya chipukizi wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50.

West Ham wameambiwa kuwa watalazimika kulipia kiasi cha pauni milioni 28 ili kumsajili Joao Mario moja kwa moja kutoka Inter Milan. (Express)

Arsene Wenger alitambua kwamba enzi za utawala wake katika klabu ya Arsenal zimefika kikomo mwezi mmoja kabla.

Watford wanatamani kumsajili beki wa Lyon, Mouctar Diakhaby, ambaye pia amekuwa akifuatiliwa na Manchester City, Chelsea pamoja na Everton.

Bodi ya klabu ya Everton itafanya mkutano wiki hii ambao unaweza kuamua hatima ya meneja wao, Sam Allardyce.

West Ham wanampango wa kuwasajili nyota wawili wa klabu ya Stoke City, Jack Butland na Joe Allen kwa pauni milioni 40 kama mahasimu wao watashuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.

Rafa Benitez anaamini matumaini makubwa ya Newcastle kumbakisha kiungo anayeichezea klabu yao kwa mkopo akitokea Chelsea, Kenedy inaweza kuwa ni kwa mkata mwingine wa mkopo. (Daily Mail)

Arsenal wataanza mkakati wa kusaka mrithi wa Arsene Wenger mapema wiki hii.

Jese Rodriguez
Stoke City wako kwenye mazungumzo na klabu ya PSG kuhusu kuvunja mkataba wa mkopo wa Jese Rodriguez baada ya nyota huyo kushindwa kuhudhuria mazoezi ya klabu hiyo. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 22 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 22 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/22/2018 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.