Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 2 Aprili, 2018
Edinson Cavani, na Angel Di Maria |
Danny Rose, Toby Alderweireld, Hector Berlin na Alex Sandro ni miongoni mwa waliopangiwa bajeti ya pauni milioni 200 na meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho. (ESPN)
Mshambuliaji wa klabu ya Monaco, Radamel Falcao anaamini teknelojia ya VAR "itaua soka" baada ya klabu yake kushindwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi nchini Ufaransa dhidi ya Paris St-Germain. (Marca)
Beki wa timu ya taifa ya Marekani na klabu ya Fulham, Tim Ream anaamini kwamba wachezaji waenye asili ya taifa hilo hubaguliwa katika soka nchini Uingereza. (Times)
Beki wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti amethibitisha kwamba Manchester United inataka kumsajili kwenye majira ya joto.
Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amesema hana tatizo na meneja Jose Mourinho na hafikirii kuihama klabu hiyo. (Manchester Evening News)
Hatima ya Robert Navarro katika klabu ya Barcelona itajulikana ndani ya siku kumi zijazo.
Nyota wa PSV, Hirving Lozano anawindwa na klabu ya Juventus ili awe mbadala wa Paulo Dybala kama ataondoka. (Sport)
Alan Pardew |
Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea, Gianluca Vialli anasema kuwa atashangaa kuona Antonio Conte akiendelea kuino klabu hiyo msimu ujao. (Sky Sports)
Vigogo wa La Liga, Real Madrid na Barcelona wanepunguza kasi yao ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah.
Jose Mourinho hatadumu kwa muda mrefu katika klabu ya Manchester United kama ataendelea kukosoa wachezaji wake, kwa mujibu wa aliyekuwa meneja wa United, Tommy Docherty. (Express)
David Moyes amesema kuwa hajaamua kama West Ham itajaribu kumsajili moja kwa moja nyota wa Inter Milan, Joao Mario kwenye majira ya joto. (Times)
Dusan Tadic anakiri kuwa anajisikia aibu baada ya Southampton kufungwa na West Ham.
Mauricio Pochettino anasisitiza kwamba Tottenham inahitaji kupata ushindi mara kwa mara katika sehemu kama Stamford Bridge kwa lengo la kuongeza hali ya kujiamini.
Arsene Wenger anatumaini kwamba, kuendelea katika hatua ya mbele kwenye Ligi ya Europa kutairejesha imani ya mashabiki wa Arsenal. (Daily Mail)
Porto wanajiandaa kumuuza mchezaji wao kutoka taifa la Mali, Moussa Marega, ambaye amekuwa akifuatiliwa na Everton, Swansea na West Ham. (Mirror)
Antonio Conte hahofii hatima yake Stamford Bridge, akisistiza kuwa yeye pamoja na wachezaji wa Chelsea 'wanajito kwa kila msimu huu' kuhakikisha timu yao inasonga mbele. (Telegraph)
Baada ya Thomas Tuchel kuipotezea ofa ya kukinoa kikosi chao, Bayern Munich wamemgeukia mkufunzi wa klabu ya Frankfurt, Niko Kovac. (Bild)
Pep Guardiola amesema kuwa hana uhakika kama Sergio Aguero atakuwa fit kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya Manchester City na Liverpool.
Loris Karius amesema kuwa hajutii kuondoka Manchester City mwaka 2011 kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool.
Matajiri wa West Brom wamehaidi kufanya mabadiliko makubwa katika klabu hiyo kwenye majira ya joto. (Sun)
Sporting Lisbon tayari iko kwenye uchunguzi wa mtu atakayechukua nafasi ya kocha wao, Jorge Jesus, huku mreno huyo akiendelea na kibarua chake cha kuinoa klabu hiyo.
Beki wa klabu ya Celtic, Kristoffer Ajer anawindwa na klabu ya Ligi Kuu ya Ujerumani, Borussia Dortmund.
Celtic wako tayari kuanza mzungumzo ya kiofisi na Scott Bain juu ya makataba wa kudumu. (Record)
Sporting Lisbon tayari iko kwenye uchunguzi wa mtu atakayechukua nafasi ya kocha wao, Jorge Jesus, huku mreno huyo akiendelea na kibarua chake cha kuinoa klabu hiyo.
Beki wa klabu ya Celtic, Kristoffer Ajer anawindwa na klabu ya Ligi Kuu ya Ujerumani, Borussia Dortmund.
Golikipa wa Dendee, Scott Bain anayeidakia Celitic kwa mkopo |
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 2 Aprili, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
4/02/2018 11:35:00 AM
Rating: