Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 30 Aprili, 2018

Antoine Griezmann
Antoine Griezmann ameamua kuwa anataka kuichezea Barcelona msimu ujao kwa sababu ya ukame wa mataji, lakini Barcelona inasita kulipa kiasi cha pauni milioni 88.08 kumnasa mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid. (Sport)

Lazio bado haijapokea ofa yoyote kutoka Real Madrid na Barcelona kwa ajili ya kiungo wao, Sergej Milinkovic, kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Igli Tare. (Premium Sport)

Mkufunzi wa klabu ya Nice, Lucien Favre anapewa nafasi kubwa ya kuwa meneja mpya wa Borussia Dortmund. (Kicker)

Klabu ya Tottenham ilikaribia kumsajili Karim Benzema kutoka Lyon kabla hajiunga na Real Madrid. (ESPN)

Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino amekubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Christian Benteke amesema kuwa anataka kubaki katika klabu ya Crystal Palace msimu ujao.

Jose Mourinho anasema kuwa Marouane Fallain anakaribia kusaini mkataba mpya katika klabu ya Manchester United.

Arsenal na Chelsea wanamfuatilia kiungo wa klabu ya Atalanta, Bryan Cristance.

Christian Fuchs
Christian Fuchs amethibitisha kuwa ataondoka Leicester City wakati mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu wa 2018/19. (Sky Sports)

Carlo Ancelotti ameripotiwa kukataa ofa ya kuwa meneja wa timu ya taifa ya Italia na kuacha milango wazi kwa klabu ya Arsenal.

Roberto Mancini ndio anayepewa nafasi kubwa ya kuwa mkufunzi wa Italia baada ya uamuzi wa Ancelotti.

Chipukizi wa klabu ya Ajax, Matthijs de Ligt amesema hana taarifa kama Spurs inamhitaji.

Wayne Rooney anadai Sam Allardyce asingeweza kufanya zaidi ya alichofanya katika klabu ya Everton na anastahili sifa - licha ya kwamba mashabiki wa klabu hiyo wanahitaji aondoke.

West Brom inakabiliana na vita ya kumbakisha Craig Dawson, huku Burnley, Wolves na West Ham zikimchunguza beki huyo.

Joey Barton anatarajia kumteua aliyekuwa mchezaji mwenzake wa QPR, Clint Hill kuwa msaidizi wake.

Meneja wa Nottingham Forest, Aitor Karanka ana tamani kumbakisha straika anayeichezea klabu hiyo kwa mkopo kutoka Cardiff City, Lee Tomlin kwa mkataba wa kudumu. (Mirror)

Mason Mount
Klabu ya Ajax inataka kumsajili kiungo wa Chelsea anayeichezea Vitesse kwa mkopo, Mason Mount kwenye majira ya joto.

Bournemouth imeingia kwenye vita ya kumsajili beki wa Celtic, Kieran Tierney, ambaye pia anawindwa na Manchester United pamoja na Tottenham.

Huddersfield wako tayari kumsajili beki kutoka Ujerumani, Leon Balogun anayeichezea Mainz. (Sun)

Dusan Tadic ameishauri Southampton imbakishe Mark Hughes kama meneja wao, hata kama klabu hiyo itashuka daraja Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.

Ben Foster anataka Darren Moore apewe mkataba wa kudumu katika klabu ya West Brom. (Telegraph)

Zeljko Buvac amejiuzulu kibarua chake kutoka benchi la ufundi la Liverpool baada ya kutofautiana na Jurgen Klopp. (Record)

Polisi katika mji wa Roma nchini Italia watapeleaka zaidi ya askari 2,000 kwa ajili ya kuwalinda mashabiki wa Liverpool kwa mashambulizi kutoka mashabiki wa A.S Roma kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano. (Daily Mail)

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane anasistiza kwamba Gareth Bale na Karim Benzema watabaki katika klabu hiyo kwenye majira ya joto. (Star)

Steven Gerrard
Steven Gerrard anatarajiwa kufanya mazungumzo zaidi juu ya kuwa meneja wa Rangers lakini bado hajafikia makubaliano na klabu hiyo. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 30 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 30 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/30/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.