Loading...

Wachezaji ambao Unai anatarajia kuwatumia kama nguzo Arsenal


Unai Emery wa Sevila amethibitishwa kuwa Kocha mpya wa Arsenal baada ya tetesi zilizoenea kwa zaidi ya saa 24 zilizopita.

Akizungumza baada ya kutambulishwa Unai alisema; “Nimefurahi sana kujiunga na klabu kubwa kwenye soka. Arsenal inajulikana na inapendwa sana duniani kutokana na staili yake ya mchezo.

“Inathamini wachezaji vijana, ina uwanja mzuri na hata inavyojiendesha imekuwa ikivutia wadau wengi sana ulimwenguni, ninajiskia raha sana kujiunga na jumuiya hii,”alisema.

“Ninaanza historia mpya ndani ya Arsenal.”

Hata hivyo, upepo ulibadilika juzi na sasa kocha huyo ambaye ameipa PSG makombe yote ya ndani msimu uliopita lakini mwishoni mwa msimu akatimuliwa.

Unai Emery ameuambia uongozi wa Arsenal kwamba ana mpango wa kujenga timu mpya kwa kutumia nguzo mbili, yaani Aaron Ramsey na Pierre-Emerick Aubameyang, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 46 amethibitishwa kuwa Kocha mpya wa Arsenal leo hii baada ya kuuvutia uongozi wa klabu hiyo kwenye mahojiano. Mikel Arteta amekuwa akihusishwa na kibarua hicho, lakini washika bunduki hao wameamua kuchagua mkufunzi mwenye uzoefu mkubwah.

Kwa mujibu wa taarifa ya The Sun, Emery aliwasilisha maelezo ya uchambuzi wa uwezo wa kila mchezaji mbele ya bodi ya Arsenal wiki mbili zilizopita.

Na wakati wa mahojiano na uongozi wa klabu hiyo, Emery aliweka wazi kwamba Ramsey na Aubameyang watakuwa wachezaji tegemezi kwenye kikosi chake msimu ujao.

Ripoti zinadai kwamba mkurugenzi wa michezo wa Arsenal, Ivan Gazidis na timu yake ya usajili waliachwa midomo wazi na maelezo ya Emery na uelewa wake mkubwa kuhusu kikosi hicho.

Chanzo cha karibu na Arsenal kililiambia The Sun: Anajua zaidi kuhusu kikosi cha Arsenal na unadani kuhusu njia waliyopita hadi kufika pale pamoja na historia ya majeruhi kwa miaka mingi.

Hawakujua ni wapi alikopata habari zile lakini walivutiwa na mkakati alioufikisha mbele yao.’

Aubameyang amekuwa na wakati mzuri tangu atue Arsenal kwa pauni milioni 56 akitokea Borussia Dortmund kwenye dirisha la usajili mwezi Januari.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alifunga magoli 10 katika michezo 13 ya Ligi Kuu ya Uingereza na anatarajiwa kuiongoza safu ya usambuliaji ya klabu hiyo msimu ujao.

Wakati huo huo, Ramsey, amebakiwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa na Arsenal, wakati wakala wake akidai kuwa mazungumzo ya mkataba mpya bado hayajaanza.

Ripoti nyingine zinadai kwamba Arsenal watamuuza Ramsey kwa pauni milioni 50 kuongeza fedha zaidi kwa ajili ya bajeti ya usajili.

Lakini inaonekana kwamba Emery ana hamu ya kumbakisha raia huyo wa Wales katika klabu hiyo.
Wachezaji ambao Unai anatarajia kuwatumia kama nguzo Arsenal Wachezaji ambao Unai anatarajia kuwatumia kama nguzo Arsenal Reviewed by Zero Degree on 5/23/2018 02:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.