Loading...

Ronaldinho 'anafunga ndoa' na wanawake wawili kwa wakati mmoja?


Aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil, Ronaldinho anaripotiwa kuwa anataka kufunga ndoa na wapenzi wake wawili kwa wakati mmoja.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 katika hali ya kushangaza, anaishi na wapenzi wake wawili Priscilla Coelho na Beatriz Souza kati jumba lake la kifahari lenye thamani ya pauni milioni 5 mjini Rio de Janeiro, na wanafanya mpango wa kupiga hatua nyingine - na wote wawili mwezi Agosti.

Ronaldinho, ambaye jina lake ni Ronaldo de Assis Moreira, atafunga ndoa na wapenzi wake wawili kwenye sherehe ya siri katika jumba lake, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka Brazil.

Kuoa mke zaidi ya mmoja ni kosa nchini Brazil, na adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka sita jela, hata hivyo inaonekana kwamba 'ndoa' hiyo ya ajabu itakuwa ni tafrija fupi tu pamoja na wanawake wawili na sio kusajiliwa kama ndoa mbili rasmi.

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona alianza uhusiano wake na Beatriz mwaka 2016, lakini aliendelea kubaki kwenye uhusiano na Priscilla, ambao ulianza mapema miaka kadhaa iliyopita.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, wapenzi wote wawili wanapata karibu pauni 1,500 kutoka kwa mwanasoka huyo kwa ajili ya matumizi yao binafsi.

Pia aliripotiwa kuwa na tabia ya kuwapa zawadi za aina moja mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na kuwanunulia manukato ya aina moja wakati wa safari yao ya pamoja nje ya nchi.


Ronaldinho aliomba kufunga pingu za maisha na wote wawili mwezi Januari mwaka jana na kuwapa wote pete za uchumba, kwa mujibu mwandishi wa makala, Leo Dias wa gazeti la 'O Dias' nchini Brazil.

Dada wa nyota huyo, Deisi, ambaye yuko anapinga kitendo hicho cha kaka yake kuoa wake wawili, tayari ameshasema hatahudhuria sherehe hiyo, kwa mujibu wa Dias.

Hata hivyo, wakati uvumi wakuwavisha pete wapenzi wake wote ulipoanza kuenea mwaka jana, Ronaldinho alikana.

''Usiamini kitu chochote kunachoandikwa kwenye habari, siku nitakapoamua kumvisha pete mchumba wangu nitawaeleza,'' aliandika nyota huyo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Licha ya kukanusha uvumi huo, kuna tetesi zinasambaa kwa kasi kuhusu sherehe hiyo inayokujwa, huku vyombo vya habari vya Brazil vikidai kuwa mwimbaji kutoka Brazil, Jorge Vercillo, ambaye ni rafiki jirani yake na Ronaldinho, amethibitishwa kuwa muhisika wa shughuli yote ya burudani siku hiyo.

Ronaldinho aliripotiwa kuomba kufnunga ndo na wawili hao Priscilla Coelho, kushoto, na Beatriz Souza, kulia mwezi Januari mwaka jana, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Brazil
Priscilla na Beatriz wote wanatoka Belo Horizonte, mji ambao nyota huyo alicheza akiwa na Atletico Mineiro, akiiongoza klabu hiyo kutwaa taji lake la kwanza la Copa Libertadores mwaka 2012.

Ingawa Ronaldinho hajawahi kuthibitisha uhusiano wake na wanawake hadharani, ameripotiwa kusafiri pamoja na wapenzi wake wote katika kila tukio analohudhuria.
Ronaldinho 'anafunga ndoa' na wanawake wawili kwa wakati mmoja? Ronaldinho 'anafunga ndoa' na wanawake wawili kwa wakati mmoja? Reviewed by Zero Degree on 5/25/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.