Loading...

Korea Kaskazini yabomoa eneo la kujaribia silaha za nyuklia

Picha ya eneo la kufanyia majaribio silaha za nyuklia Korea Kaskazini la Punggye-ri kabla ya kuharibiwa
Korea Kaskazini imeharibu mashimo yaliyo katika eneo pekee la majaribio ya silaha za nyuklia, ili kupunguza taharuki kati yake na Korea Kusini na Marekani.

Waandishi wa habari wa kimataifa katika eneo la majaribio ya silaha za nyuklia la Punggye-ri lililo kaskazini mashariki walishuhudia mlipuko mkubwa.

Pyongyang ilitangaza kusitisha shughuli zake za nyuklia mwanzoni mwa mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kidiplomasia kati yake, Korea Kusini na Marekani.

Mashimo matatu yalilipuliwa mbele ya waandishi wa habari wa kimataifa takribani 20. Milipuko miwili ilitokea asubuhi na mingine minne nyakati za jioni.

Mwanahabari wa Sky News Tom Cheshire alikuwa mmoja wa wanahabari waliokuwa kwenye eneo hilo,Amesema milango ya tunnels ilikuwa imefungwa huku ikiwa na nyaya kila mahali.

''Tulipanda milimani na kutazama shughuli hiyo umbali wa mita 500 kutoka kwenye eneo hilo''

''Walihesabu, tatu,mbili, moja, kisha ukatokea mlipuko mkubwa, uliweza kuuhisi, kulikuwa na vumbi jingi, joto kali, mlipuko ulitoa sauti kubwa."

Korea Kaskazini imekwishafanya majaribio sita ya nuklia tangu mwaka 2006 kwenye mfumo wa mashimo yaliyochimbwa chini ya mlima Mantap.

Inaaminika kuwa ni eneo pekee la majaribio duniani mpaka sasa.

Source: BBC
Korea Kaskazini yabomoa eneo la kujaribia silaha za nyuklia Korea Kaskazini yabomoa eneo la kujaribia silaha za nyuklia Reviewed by Zero Degree on 5/24/2018 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.