Loading...

Mashabiki Yanga SC wautaka uongozi kuachia madaraka


Baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga wameutaka uongozi wa klabu hiyo uliopo madarakani kuachia ngazi kutokana na mwenendo mbaya wa kikosi namna kinavyoenda hivi sasa.

Mashabiki hao wameutaka uongozi huo kuachia madaraka kufuatia mabango waliyokuwa wameyabeba wakati Yanga ilipokutana na Mbao FC katika mchezo wa ligi uliopigwa jana Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa.

Moja ya bango lilisomeka likieleza kuutaka uongozi uiachie timu huku mengine yakiwataja baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ikiwemo jina la Salum Mkemi kuwa ni moja ya maadui ndani ya Yanga.

Yawezekana pengine mashabiki hao wameamua kufanya hivyo kutokana na mwenendo wa klabu yao kutokuwa mzuri kiuchumi huku kiwango cha timu kikiwa si shwari kama siku za nyuma.

Yanga iliweza kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao jana na kuweza kufuta rekodi ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo 9 mfululizo iliyopita katika mashindano yote.
Mashabiki Yanga SC wautaka uongozi kuachia madaraka Mashabiki Yanga SC wautaka uongozi kuachia madaraka Reviewed by Zero Degree on 5/23/2018 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.